Na Walter Mguluchuma .
Katavi
Chama cha Walimu CWT Wilaya ya Mpanda kimewapatia mafunzo walimu wenye ulemavu lengo la kuwafanya watambue mahitaji yao walimu wenye ulemavu katika sehemu zao wanazofanyia kazi .
Mafunzo hayo ya siku moja yalifanika jana katika ukumbi wa chama hicho na yalifunguliwa na Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Mpanda jumanne Msomba na yaliwashirikisha walimu wote wenye ulemavu wa kutoka katika Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa sasa Tanganyika .
Katika hutuba yake ya ufunguzi Msomba aliwaeleza Walimu hao wenye mahitaji maalumu alisema CWT imeona iwapatie mafunzo hayo ili waweze waweze kufahamu mahitaji yao muhimu katika sehemu zao wanazofanyia kazi pamoja na mazingira yao ya kazi .
Lengo jingine ni kuwafanya wafahamu na kutambua mahitaji yao maalumu ya walimu wenye mahitaji maalumu kwenye maeneo yao wanayofanyia kazi na kuelimishwa sheria mbalimbali zinazo muhusu mwalimu sehemu ya kazi .
Katibi wa CWT Wilaya ya Mpanda Wilison Masolwa alisema CWT alieleza kuwa zamani watu walikuwa wakidhani kuwa mtu mwenye ulemavu hawezi kufanya jambo lolote lile wala kuongoza wakati sio kweli .
Ndio maana kwa kutambua hilo CWT imeanzisha kitengo cha walemavu ndani ya chama hicho kwa lengo la kusimami haki za walimu wenye mahitaji maalumu .
Katibu wa CWT wa Mkoa wa Katavi Luccy Masegenya alisema Sera ya CWT wamapanga kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2025 walimu wote wenye mahitaji maalumu wanafanya kazi kwenye mazingira bora .
Aliwaka kutojibagua kutokana na ulemavu wao bali wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho na nje ya Cwt ili kusaidia kuleta maendeleo ya Taifa .
Mmoja wa Walimu wenye mahitaji Maalumu Peter Pesambili alieleza kuwa walimu wenye ulemavu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye sehemu zao za kazi .
Alitaja baadhi ya changamoto kuwa wamekuwa hawatambuliwi kulingana na ulemavu wao wao katika kupangiwa vituo vyo vya kazi kwa kupangiwa maeneo ambayo wanaishi mbali na vituo vya kazi .
Pia wamekuwa wakibaguliwa kwa kutopewa madaraka kwenye maeneo yao ya kazi na hata inapotokea kwenda kusimamia mitihani wamekuwa hawachukuliwi japo wao ni wachache na wamekuwa wakipangiwa idadi sawa ya vipindi vya kufundisha sasa sawa na walimu wasio na ulemavu.
Changamoto nyingine aliitaja kuwa ni majengo wanayofanyia kazi hayakujengwa kwa kuzingatia mahitaji ya walimu na wanafunzi wenye mahitaji maalumu .
Mwakilishi wa Walimu wenye ulemavu kwenye Cwt Wilaya ya Mpanda Richald Chitambala alieleza kuwa hivi karibuni walifanya zoezi la kuwaondoa baadhi ya walimu kwenye kitengo hicho ambao wamekuwa wakijiita walemavu wakati sio walevu .
Na zoezi hilo litakuwa endelevu kwa walimu ambao wanataka kutumia vibaya kitengo hicho cha walimu wenye ulemavu .
0 comments:
Post a Comment