Friday, July 29, 2016

CHAMA CHA WALIMU MPANDA CHAWAPATIA MAFUNZO WALIMU WENYE ULEMAVU .


   Na  Walter   Mguluchuma .
          Katavi
        Chama   cha   Walimu      CWT  Wilaya  ya   Mpanda kimewapatia   mafunzo  walimu  wenye  ulemavu   lengo  la kuwafanya  watambue   mahitaji yao  walimu   wenye  ulemavu  katika  sehemu  zao  wanazofanyia   kazi .
Mafunzo  hayo ya   siku  moja  yalifanika  jana   katika  ukumbi wa   chama  hicho na yalifunguliwa  na   Mwenyekiti  wa  CWT   Wilaya  ya    Mpanda   jumanne   Msomba na  yaliwashirikisha  walimu  wote   wenye   ulemavu wa  kutoka   katika  Manispaa   ya  Mpanda   na   Halmashauri ya   Wilaya  ya   Mpanda kwa  sasa  Tanganyika .
 Katika  hutuba  yake  ya  ufunguzi  Msomba   aliwaeleza  Walimu  hao   wenye   mahitaji  maalumu   alisema   CWT  imeona   iwapatie   mafunzo  hayo  ili waweze  waweze   kufahamu  mahitaji yao  muhimu  katika   sehemu  zao wanazofanyia  kazi  pamoja  na   mazingira yao ya  kazi .
Lengo  jingine  ni  kuwafanya    wafahamu  na  kutambua   mahitaji  yao  maalumu   ya  walimu   wenye   mahitaji  maalumu  kwenye  maeneo yao  wanayofanyia  kazi  na  kuelimishwa  sheria  mbalimbali  zinazo  muhusu    mwalimu  sehemu  ya  kazi .
  Katibi  wa  CWT   Wilaya  ya   Mpanda   Wilison     Masolwa  alisema   CWT    alieleza  kuwa     zamani  watu walikuwa  wakidhani  kuwa   mtu  mwenye   ulemavu  hawezi  kufanya  jambo  lolote  lile  wala kuongoza  wakati  sio  kweli .
Ndio    maana  kwa  kutambua  hilo   CWT   imeanzisha  kitengo   cha   walemavu   ndani  ya    chama  hicho  kwa   lengo la kusimami  haki za   walimu   wenye   mahitaji   maalumu .
Katibu  wa   CWT  wa     Mkoa  wa   Katavi   Luccy   Masegenya   alisema    Sera  ya   CWT   wamapanga  kuhakikisha    hadi  kufikia   mwaka   2025  walimu  wote  wenye  mahitaji  maalumu  wanafanya   kazi  kwenye  mazingira  bora .
 Aliwaka  kutojibagua  kutokana  na  ulemavu wao   bali  wajitokeze  kugombea  nafasi  mbalimbali za uongozi  ndani ya  chama  hicho na  nje    ya  Cwt  ili  kusaidia   kuleta  maendeleo  ya  Taifa .
Mmoja  wa   Walimu  wenye  mahitaji   Maalumu    Peter  Pesambili alieleza    kuwa  walimu   wenye  ulemavu  wamekuwa  wakikabiliwa  na  changamoto  mbalimbali kwenye   sehemu  zao  za  kazi .
  Alitaja   baadhi ya  changamoto  kuwa  wamekuwa  hawatambuliwi  kulingana  na  ulemavu wao  wao  katika   kupangiwa  vituo  vyo  vya  kazi  kwa  kupangiwa  maeneo ambayo  wanaishi  mbali na  vituo  vya  kazi .
Pia  wamekuwa  wakibaguliwa kwa kutopewa   madaraka  kwenye  maeneo yao ya  kazi  na  hata  inapotokea  kwenda kusimamia  mitihani  wamekuwa   hawachukuliwi  japo   wao ni  wachache na wamekuwa  wakipangiwa  idadi  sawa ya  vipindi  vya kufundisha  sasa  sawa na walimu  wasio na  ulemavu.
  Changamoto  nyingine   aliitaja  kuwa  ni  majengo  wanayofanyia  kazi   hayakujengwa kwa kuzingatia  mahitaji ya  walimu  na  wanafunzi  wenye  mahitaji  maalumu .
Mwakilishi  wa   Walimu  wenye  ulemavu  kwenye    Cwt  Wilaya  ya   Mpanda   Richald   Chitambala   alieleza  kuwa   hivi  karibuni walifanya  zoezi  la kuwaondoa     baadhi ya  walimu  kwenye kitengo hicho   ambao  wamekuwa  wakijiita  walemavu  wakati  sio  walevu .
 Na  zoezi  hilo  litakuwa  endelevu  kwa  walimu   ambao  wanataka  kutumia  vibaya   kitengo  hicho  cha  walimu   wenye  ulemavu .

No comments:

Post a Comment