Na Walter Mguluchuma .
Katavi yetu blog
Mahakama ya Wilaya ya Wilaya ya Mpanda imemwachia huru aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Lawrence Masha pamoja na viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wa Mkoa wa Katavi baada ya Mahakama kuona hawana hatia ya kosa walilikuwa wameshitakiwa la kuingia kwenye makazi ya wakimbi ya Katumba bila kuwa na kibali .
Hukumu ya mwamwachia Masha na wenzake sita ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya upande mashitaka uliokuwa ukiongozwa na mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Lungano Mwasabila kushindwa kutowa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani washitakiwa.
Washitakiwa wengine walioachiwa huru hapo jana ni Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda Abrahamu Mapunda aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Nsimbo chadema ambae pia ni mwandishi maarufu hapa nchini Gerald Kitabu . Katibu wa Vavicha wa Mkoa wa Katavi Franco Misigari , Mwenyekiti wa Jimbo la Nsimbo Chadema Stansilaus Kaswele na katibu wa Jimbo la Nsimbo Lameck Costantino .
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Chiganga aliiambia Mahakama kuwa upande wa mashitaka katika kesi hiyo iliwafungulia washitakiwa wate saba mashitaka matatu ya kuingia kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba bila kuwa na kibali , pia walidaiwa kuingia ndani ya makazi ya katumba na bila kibali na kushawishi na walishitakiwa kwa kuingia kwenye makazi ya wakimbizi bila kibali na kufanya mkutano .
Alisema washitakiwa ambao walidaiwa kutenda kosa hilo hapo oktoba 20 mwaka jana walikana mashitaka hayo kwa kile walichodai kuwa eneo hilo sio kambi ya wakimbizi bali ni makazi hivyo hawakuwa na sababu yoyote ya kuwafanya waingie kwenye eneo hilo wakiwa na kibali cha mkuu wa Makazi .
Aliendelea kueleza pamoja na upande wa mashitaka kupeleka mashidi kumi mahakamani hapo umeshindwa kuwasilisha kielelzo kilichoombwa kiletwe mahakamani na wakili wa upande wa utetezi Filbert Msanda kutoka Dares salaam ambao walitaka waonyesha gazeti la Serikali lililotangaza kuwa eneo hilo ni la makazi ya Wakimbizi Hakimu Chiganga aliendelea kusoma hukumu hiyo kuwa mahakama imeona shaka ushahidi uliotolewa na msimamizi wa jimbo la uchaguzi wa la Nsimbo George Nzyungu alidai kuwa yeye alikuwa ndiye mwenyemamlaka ya kutowa kibali cha kuwaruhusu chadema kwenda kufanya mkutano kwenye makazi hayo wakati kwa mujibu wa sheria namba 16 ya wakimbizi .
Alieleza mahakama imeona kuwa makazi ya wakimbizi ya katumba yalianzishwa mwaka 1973 na makazi hayo yalipaswa kisheria kutangazwa na gazeti la serikali lakini haikufanyika hivyo na ya liitngazw kwa mdomo na Rais.
Hivyo kutokana na kifungu cha sheria namba 235 kidogo cha sheria mahakama imewachia huru washitakiwa kuanzia mshitakiwa wa kwanza Lawrence Masha na Washitakiwa wenzake .
Akizungumzia hukumu hiyo wakili wa washitakiwa Filbert Msanda alisema ameridhishwa na uamizi uliotolewa na Mahakama hiyo na ameomba Mahakama nyingine hapa nchini ziwe zinatowa hukumu kwa haki bila kujali mshitakiwa anatoka chama gani cha siasa .
0 comments:
Post a Comment