Na Walter Mguluchuma .
Katavi .katavi yetu blog
Kesi inayo mkabili aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Lawrence Masha akiwa na viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA waliofikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kufanya mkutano wa hadhara na kuingia bila katika makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi jana iliendelea kusikilizwa na leo itaendelea ambapo upande wa mashitaka leo umepanga kufunga kuwakilisha ushahidi wake .
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa ambapo Masha na wenzake wanatetewa na wakili Abelti Msando kutoka Deres salaam.
Masha na na watuhumiwa wenzake sita walifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Oktoba 16 mwaka jana huku wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na bunduki na mabomu ya machozi na kusomewa mashitaka na mwanasheria wa Serikali Mkoa wa Katavi Lungano Mwasubila.
Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo aliyekuwa mgombea ubunge chadema wa Jimbo la Nsimbo Gerald Kitabu, Abrahamu Mapunda mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mpanda , Franco Misigalo katibu wa Bavicha Mkoa wa Katavi , Stansilaus Kaswele Mwenyekiti Chadema jimbo la Nsimbo na Lameck Costantino katibu wa Chadema jimbo la Nsimbo .
Masha ambae ni mshitakiwa wa kwanza wanadaiwa kuwa Oktoba 19 mwaka jana majira ya saa saba mchana wote kwa pamoja walitenda kosa hilo katika makazi ya wakimbizi ya Katumba .
Washitaki katika kesi hiyo inayoendelea kusililizwa na kuvutia hisia za watu wengi wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi wanakabiliwa na tuhuma za mashitaka matatu .
Shitaka la kwanza ni lakuingia ndani ya makazi ya wakimbizi bila kibali cha mkuu wa makazi ya Katumba na shitaka la pili kuingia ndani ya makazi ya wakimbizi bila kibali na kufanya mkutano wa hadhara na shitaka la tatu kuingia kwenye makazi ya wakimbizi bila kibali cha Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi.
Upande wa mashitaka jana uliendelea kutowa ushahidi wake na kesi hiyo imepangwa kuendelea hapo leo ambapo upande mashitaka utakuwa unafunga towa ushahidi wake .
Masha na washitakiwa wanzake ambao wote walikuwepo Mahakamani wanaendelea kuwa nje ya mdhamana baada ya kutimiza masharti ya mdhamana toka hapo awali walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza
0 comments:
Post a Comment