Na Walter Mguluchuma.
Katavi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Alex Kaguze amewaagiza watumishi wa Halmashauri hiyo kuwa karibu na Wananchi ili wawze kubaini na kutatua kwa haraka kero zinazowakabili Wananchi bila kusukumwa na viongozi .
Kaguza alitowa agizo hilo hilo hapo jana wakati wa mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlele Godwin Benne ambae amestaafu ,
Alisema kuwa katika Halmashauri hapa Nchini h kuna hari ambayo imezoweleka ya watumishi kutowafikia Wananchhi kwa wakati kitendo ambacho kimekuwa kikipelekea Wananchi kukosa huduma stahiki ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya jamii.
Aliongeza kuwa miongoni mwa kero zinazowakabili wananchi ni pamoja na kukosekana kwa huduma za afya , Maji safi , Elimu bora na miundo mbinu mbalimbali .
Alisema endapo watumishi hawaka kuwa karibu na wananchi itakuwa sio jambo rahisi kwao kutatua changamoto ambazo zinawakabili wananchi katika Halmashauri hiyo .
Kwa upande wake aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Godwin Benne aliwataka watumishi watowe ushirikiano kwa mkurugenzi huyo mpya kama walivyokuwa wakimpatia yeye kwa kupitia kaulimbiu ya Mlele bila umaskini inawezekana twende pamoja .
Benne pia aliwaomba watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kulinda heshima iliyopewa Halmashauri ya Mlele kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo ya kupata hati safi na ushindi katika Nyanja mbalimbali ikiwa na pamoja na mbio za Mwenge 2014 na 2015 kimkoa na kikanda ,Kiwango cha ufaulu kwa Elimu ya Msingi na Sekondari .
Nae mwakilishi wa Watumishi wa Halmashauri hiyo Seif Makome ambae ni mkuu wa Idara ya Mipango takwimu na ufuatiliaji alimshukuru mkurugenzi aliyestaafu Godwin Benne kwa uchapakazi wake katika kipindi cha uongozi wake katika kipindi cha miaka mitatu aliyoingoza Halmashauri ya Mlele.
Alisema Halmashauri ya Mlele ilianzishwa mwaka 2013 Julai chini ya Mkurugenzi Mtendaji Godwin Benne ambapo hadi sasa Halmashauri hiyo imetimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake na imekuwa ni miongoni mwa Halmashauri ambayo imepiga hatua za Maendeleo.
0 comments:
Post a Comment