Home » » BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA VIFAA KWA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KATAVI

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA VIFAA KWA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na         Walter  Mguluchuma  Na   Irine  Temu    Katavi .
Katavi yetu blog
Benki ya  NMB imetowa  msaada wa vifaa vitendea  kazi  kwa  Chama  cha  Waandishi wa  Habari Mkoa wa  Katavi KTVPC  vyenye  thamani ya  zaidi ya shilingi Milomi 5.8 vitakavyo wasaidia  waandishi wa  Habari ambao ni wanachama wa  chama  hicho kufanya  kazi kwa ufanisi mkubwa .
Msaada huo wa vifaa  hivyo ulikabidhiwa  hapo  jana  katika  ofisi za  Chama  cha Waandishi wa  Habari  Mkoa  wa  Katavi  zilizopo  katika  mtaa wa   Madukani  ambapo   mgeni  rasmi wakati wa  makabidhiano  hayo  alikuwa  ni mkuu wa  Mkoa wa  Katavi  Meja  Jenerali Mstaafu  Raphael  Muhuga.
 Awali  kabla ya kukabidhi   vifaa  hivyo  Meneja wa  NMB  Tawi la  Mpanda     Happines  Pimma  alieleza kuwa Benki ya  NMB  inatambua   mchangowa  waandishi wa  Habari  katika kuelimisha  jamii.
 Alisema kwa kutambua   umuhimu wa  waandishi na   kuthamini  mchango wao ndio  maana wameamua kutowa msaada wa  vifaa vitendea kazi kwa ajiri ya  chama  cha waandishi wa  Habari  Mkoa wa  Katavi ili viweze kuwasaidia waandishi wa  Habari ambao ni  wanachama wa  Chama  hicho .
Happiness alivitaja  vitendea  kazi  zilivyotolewa  na  Banki ya  NMB kwa  chama  cha  Waandishi wa  Habari Mkoa wa  Katavi  kuwa  ni   Deski  Topu Kompyuta  nne  Lap Topu  moja  na  printa  moja  vyote  vikiwa  na  thamani ya   shilingi Milioni 5.8.
 Alisema    NMB  imekuwa  ikitowa  misaada mbalimbali  kwenye  jamii na   ndio taasisi ya   Kibenki Inayoongoza  hapa   nchini kwa kutowa  misaada  mingi  kwenye  jamii   hapa  Nchini.
Mkuu wa  Mkoa  wa  Katavi  Meja  Jenerali  mstaafu  Raphael  Muhuga   alisema  kuwa  msaada huo uliotolewa   na  Benki  ya NMB   kwa  chama  cha  Waandishi wa  Habari   cha  Mkoa  wa  Katavi si  haba .
  Alisema  msaaada  huo  unauhakika  utasaidia   kupunguza   tatizo  la  uhaba   kwa    vifaa  vya kutendea  kazi  kwa  Waandishi  wa  Habari  ambao ni   wanachama   wa   chama  hicho ,
 Alifafanua  kuwa  waandishi wa  Habari  Mkoani  Katavi   wamekuwa  ni  chachu  kubwa ya kuleta  maendeleo  kwa  wananchi  wa  Mkoa huu kwani  wamekuwa  wakifikisha  kwa  haraka  sana  taarifa   zinazokuwa  zinatolewa  na  viongozi wa  Serikali  hasa  kwenye  yale  maeneo  ambayo  viongozi wamekuwa  hawafiki kwa wakati huo ila taarifa   zimekuwa zikiwafikia  wananchi .
  Muhuga   pia  aliiomba    NMB  kuangalia    uwezekano  wa  kukipatia  vifaa  vya  aina  nyingine   chama  hicho  cha waandishi wa   Habari    Mkoa  wa  Katavi  kwani  yeye  bado  anaamini  kuwa   chama  hicho    bado ni  kichanga   bado  hakija jitosheleza  hivyo  bado  kinahitaji msaada  zaidi .
Mwenyekiti wa  Chama  cha  Waandishi wa  Habari  Mkoa  wa   Katavi  Walter  Mguluchuma  aliishukuru   NMB kwa kutowa  msaada  huo ambao  utasaidia  sana  kupunguza  tatizo la  vitendea  kazi kwa   wanachama wa  chama  hicho .
 Alisema  waandishi  wengi wa  Habari  sio wa  ajiriwa  bali ni wakujitegemea  hivyo wamekuwa  hawana  uwezo wa kifedha  wa kununulia  vitendea  kazi     hivyo  vifaa walivyopewa   vitawasaidia  kufanya  kazi zao kwa  urahisi  na  kufanya  kazi kwa  wingi kwa  wakati mmoja  tofauti  na  hapo  awali .
  Pia  alitowa  wito  kwa   Taasisi  nyingine,Mashirika  na  watu  binafsi  kuiga   mfano huo wa  NMB   kwa  msaada huo waliotowa  na    milango  iko  wazi kwa  chama  hicho kwa  kupokea  msaada wa  ina  yoyote ile .
Nae  Meya wa  Manispaa ya  Mji  wa   Mpanda    Willy  Mbogo   aliwapongeza  waandishi  wa   Habari  wa  Mkoa  wa  Katavi   kwa  jitihada  kubwa  wanazofanya  za  kuutangaza  Mkoa  huo   tofauti  na  apo  awali .
  Alisema  yeye  ni  mdau  mkubwa  wa  vyombo  vya   habari  na  amekuwa   akifatilia  sana  kusoma   magezeti  kusikiliza  radio  na  kuona    Tv  na  kila  siku  zimekuwa  zikitoka   habari  za  kutoka   Mkoa wa  Katavi    hivyo   hatuna   budi  kuwapongeza  waandishi wa   Habari kwa  kazi kubwa  wanayo  fanya .
Katika  Hafra  hiyo   Meya  huyo wa  Manispaa  ya  Mpanda amlihaidi  kulipia  gharama ya  kodi ya  ofisi ya  chama  cha  waandishi wa  Habari Mkoa wa  Katavi  kodi ya  mwezi  mmoja  na  Mwandisi wa  Tan    roods Martini  Mwakabende alihaidi  kutowa  msaada  wa malipo ya   mshahara  ya  mlinzi  ya  mwezi  Julai.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa