Home » » ZAIDI YA MILIONI 56 ZA MISHAHARA HEWA ZAREJESHWA KATAVI

ZAIDI YA MILIONI 56 ZA MISHAHARA HEWA ZAREJESHWA KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


  Na  Walter  Mguluchuma
                    Katavi
Zaidi ya   shilingi  milioni  56  zimerejeshwa  Mkoani  Katavi   hadi sasa   katika  ya zaidi  ya    shilingi   Milioni   240.3 zilizolipwa  kama  mishahara  hewa  katika  Mkoa  wa  Katavi kiasi  hicho  kilichorejeshwa  ni  sawa  na   asilimia  23.3.
Fedha  hizo  zimerejeshwa  kufuatia  agizo lililotolewa  na  Mkuu wa  Mkoa  wa  Katavi   Meja  Jenerali  Mstaafu  Raphael  Muhuga alilolitowa   kwa  Wakurugenzi wote wa  Halmashauri za  Mkoa wa  Katavi  la  kuwataka    wahakikishe   fedha  zote  walizolipwa  watumishi  hewa   46  waliobainika   katika  Mkoa wa  Katavi zinarejeshwa  Serikalini .
Mkuu wa  Mkoa wa Katavi   Meja Jenerali   mstaafu  aliwaambia  Waandishi  wa  Habari jana   ofisini  kwake  kuwa   hadi  sasa  kiasi  cha  shilingi  56,1o2,900  zimerejeshwa   kati ya  shilingi  milioni  240,369,257 zilizolipwa   kama   mishahara  hewa   katika  Mkoa  wa  Katavi  kiasi  hicho  ambacho  ni  sawa na  asilimia   23.34.
 Alisema   hadi  kufikia   Mei  4  mwaka  huu   Mkoa  wa  Katavi ulikuwa  na  idadi ya  watumishi  hewa   46 ambao  walibainika  wakiendelea  kuchukua  mishahara  wakati hawasitahili  na kuitia   hasa   Serikali  kiasi  cha   shilingi Milioni  200,792,448.
Alifafanua  kuwa  watumishi  waliokufa  lakini  walikuwa wakiendelea  kulipwa  mishahara walibainika  watano, watumishi waliostaafu  19, walioacha  kazi  kwa  hiari  lakini walikuwa  wakilipwa alibanika  mmoja , waliokuwa  na  mishahara  miwili  wawili, watumishi  ambao  ni watoro  sugu   na  hawapo  vituoni 13.
 Watumishi  waliokuwa  na  vyeti  vya kugushi  ambao  walikimbia na kutokomea kusiko  julikana    baada ya  timu aliyoiunda kuanza kufanya  kazi  ni watatu  na  watumishi waliofukuzwa  kazi  na  kuendelea  kulipwa  mishahara  ni  watatu .
Meja   Jenerali  Mstaafu  Muhuga  alisema  Manispaa ya   Mpanda   ambayo ilibainika kuwa na     idadi ya  watumishi  hewa 16   hadi  june  20 ilikuwa  imerejesha  kiasi   cha   shilingi   Milioni 24,841,899 kati ya  Tsh 69,917216, Halmashauri  ya  Nsimbo  yenye  watumishi  hewa 11  hadi  sasa  imerudisha   Tsh 9,306,800  kati ya  Tsh  90,661,880.
  Halmashauri ya  Wilaya  ya  Mpanda walibainika  watumishi  hewa  tisa      na wamerejesha  kiasi  cha  shilingi milioni 12,674,201  kati ya  shilingi   milioni  33,759,041  na  Halmashauri  ya Wilaya  ya  Mlele  yenye  watumishi hewa    tisa  wamerejesha  kiasi  cha  shilingi  milioni 9,280,000  kati ya   shilingi  milioni   46,031,120.
Mkuu  huyo  wa  Mkoa   alieleza  kuwa   kuhusu  watumishi  hewa  15  ambao   taarifa  zao   zina   utata , uchunguzi   bado  unaendelea   ambapo   TAKUKURU   inasaidia   fuatilia  ili  kuhakikisha   taarifa  muhimu   ambazo  tume  aliyoiunda  ilishindwa   kuzipata  kwa  baadhi ya  watumishi  kutokana  na  taratibu za   kisheria   katika  Benki ya  NMB zinapatikana

Muhuga  alisema  zoezi  hilo  la  urejeshwaji wa  fedha  za   mishahara  hewa   bado   linaendelea  katika   Halmashauri  zote  za   Mkoa  wa  Katavi na  watumishi  hewa  waliobainika  katika   Mkoa wa   Katavi   tayari wamefutwa  kwenye   orodha ya  watumishi  wanaolipwa   mishahara .
Na  baada  ya  kukamilika  kwa  urejeshwaji  huo   ndipo   maafisa  utumishi  wote  ambao  wakakao  bainika  kuhusika   na  mishahara  hewa  watachukuliwa  hatua  za  kinidhamu za  kiutumishi  pamoja  na  watumishi  walioshirikiana   nao .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa