Home » » TANAPA KUBADILI UTENDAJI WAKE WA KAZI NA KUWA WAKIJESHI

TANAPA KUBADILI UTENDAJI WAKE WA KAZI NA KUWA WAKIJESHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

  Na  Walter  Mguluchuma
       Katavi 
Shirika  la  Hifadhi la  Wanyama   pori  Tanzania  TANAPA  Lipo  kwenye utaratibu  wa kubadili    mfumo wa utendaji  kazi  kutoka  mfumo wa awali  wa kiraia  na kuingia  kwenye mfumo  wa Kijeshi USU  ilikukabiliana  na  hari ya sasa ya ujangili.
Hayo  yalisemwa  hapo  jana  na   Katibu  Mkuu wa  Wizara ya  Maliasi na utalii  Meja Generali   Gaudensi  Milanzi wakati  alipokuwa akifunga  mafunzo ya miezi mitatu ya    Askari 14 wa  TANAPA   wa  ngazi  mbambali  katika  chuo cha  wanyama  pori cha  Mlele   Mkoani  Katavi .
Meja   Generali  Milanzi  alisema  mabadiliko  hayo  ya kimfumo  ni  matakwa  ya  sheria  ya uhifadhi  wa  wanyama  pori  Na  5 ya  mwaka  2009 kifungu  namba 10,11, 12  na  13 ambayo  imeanisha  wazi  kwamba  ili  kuhakikisha  ulinzi  kamili wa  maliasili  katika   maeneo  yaliyohifadhiwa ,kutaundwa  kikosi  cha  jeshi USU(pa
 Aileleza kuwa  Askari wa  TANAPA  wamekuwa wakuwa wakifanya kazi kiraia  wakati majangili walioko   kwenye  hifadhi za  Taifa na  kwenye  mapori ya akiba wanatumia  silaha za kivita hari  ambayo  imekuwa  ikipelekea  ugumu wa  kiutendaji wa kazi .
Aidha ni imani yake kuwa  kupitia  mafunzo walioyapata  askari  hao  wamejifunza  mengi  yanayohusiana  na  dhana  nzima  ya uongozi  na  nidhamu   haswa  katika  kipindi  hiki  ambacho  uhifadhi  unashuhudia  mmomonyoko mkubwa  wa  maaadili  kwa watumishi ,ujangili wenye  kutumia   mbinu  za kisasa  mfano  tukio la  hivi  karibuni  la  majangili  kuipiga  na kuidondosha   helikopita  iliyokuwa  inafanya   doria   katika  pori la maswa  ambao ulihusisha watumishi wa sekta ya uhifadhi.
 Alisema Taifa  kwa  kipindi  cha  hivi  karibuni  ilmeshuhudia  mmomonyoko   mkubwa  sana  wa  maadili  kwa watumishi  wake  haswa wa ngazi  ya  askari  hivyo aliwaomba wahitimu  hao  wawe  kioo na  kielelezo  kizuri  cha  uhifadhi  katika  vituo vya kazi .
Mkuu wa  Mkoa wa Katavi  Meja Genarali  Mstaafu  Raphael  Muhuga alisema wale  wote  ambao walikuwa wanajihusisha na ujangili na kuingiza mifugo yao  katika   hifadhi ya Taifa  ya  Katavi watambue  kuwa wakati  wao kwa sasa umekwisha .
 Alisema  viongozi wa siasa  wamekuwa wakiingilia  mara kwa mara  zoezi la operesheni la  kuhamisha watu wanao vamia  maeneo ya  hifadhi kwa  kisingizio cha kuwazingizia  askari wanaofanya   zoezi la kuwahamisha  wavamizi kuwa kuwa wakati wanapokuwa wanafanya zoezi hilo huwa wanabaka  yeye  kama  Mkuu wa  Mkoa  hatakuwa  tayari   kuona  mali asili zinahujumiwa  katika  Mkoa  wake .
Na  ataendelea kushirikiana  na  TANAPA kuhakikisha   mifugo  yote ambayo  imeingia  kwenye  hifadhi inaondolewa na amewaagiza  viongozi wa  serikali za vijiji kutenga  maeneo ya matumizi  bora ya  ardhi.
Nae  Mkurugenzi  Mkuu wa   shirika  la  TANAPA  Alan Kijazi alisema  TANAPA  imejipanga  kuhakikisha  inatowa   mafunzo  mbalimbali  kwa  askari wake  ili kuweza  kukabiliana   na  swala  zima  la ujangili  hapa  Nchini.
 Alisema  mafunzo  hayo  waliopata wahitimu hao  ni  muhimu  sana kwa askari wa  TANAPA   na  yanatokana  na  kukabiliana  na  hari  kubwa ya  ujangili  ambao  sasa  hivi umechukua  sura  nyingine  kutokana na  majangili kuanza kutumia  silaha za kisasa  zaidi .
Aliiomba Wizara ya  Mali  Asili  na  utalii izifanyie  kazi  changamoto  zote za  shirika  la  TANAPA  ililiweze    kufanya  kazi zake za kwa  ufanisi  mkubwa  na  kuendelea kulinda  rasilimali za  nchi  yetu .
Alisema  mafunzo  katika  chuo  hicho yatakuwa ni endelevu kwani wanatarajia kufanya  mafunzo mengine  hivi  karibuni kwa ajiri ya   mameneja  wa  makao  makuu  na wahifadhi wakuu ambao jumla yao 21  ilikuimarisha  mfumo  huo wa   jeshi Usu na  baada ya  mafunzo hayo  kwa viongozi  kumalizika  wataanza  mafunzo  kwa  askari wote wa  TANAPA.
 Kaimu    Meneja  wa  mapori ya  akiba  ya  Rukwa  Lwafi   Mark  Chuwa   alisema  kuwa   Idara ya wanyama  pori   na  hifadhi za Taifa  waliisha  kukubaliana  kushirikiana  kukuza  utalii  hapa   nchini .
Msoma  risala  ya  wahitimu  hao  Stela  Mwangoka   alieleza  kuwa   mafunzo  hayo ni mojawapo ya  hatua   muhimu ya  shirika  la  hifadhi za  Taifa   Tanzania  kutekeleza   muundo  mpya  wa kurugenzi  ya uhifadhi  wa kuingia   katika  mfumo wa  jeshi  Usu ambao kwa sasa  unatumika   kwenye  Taasisi   nyingi  za  kiuhifadhi   katika  Bara  la  Afrika na  pia  katika  kutekeleza   sheria  elekezi kwa Taasisi za uhifadhi wanyama  pori  Tanzania.
Alisema   mafunzo  hayo  yaliwashirikisha  pia  wahifadhi   mbalimbali  na  makao  makuu ya  shirika   katika  mafunzo hayo  ya  awamu ya  tano  Wahifadhi 26 ni  wahifadhi  wafawidhi,wahifadhi wandamizi  na  wahifadhi  wasaidizi   na  askari    wa  ajira  mpya wa  TANAPA 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa