Home » » TAKUKURU YAMPANDISHA KIZIMBANI MKURUGENZI WA HALMASHAURI NA MWANDISI WA UJENZI

TAKUKURU YAMPANDISHA KIZIMBANI MKURUGENZI WA HALMASHAURI NA MWANDISI WA UJENZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
  Katavi
Taasisi ya  kuzuia na  kupambana  na  Rushwa  TAKUKURU  Mkoa wa Katavi imewapandini sha  kizimbani katika  Mahakama ya  Wilaya ya  Mpandai Mkurugenzi wa  Halmashauri ya  Wilaya ya  Serengeti   Naomi  Nko   na  godfrey  Majuto  mwandisi wa Manspaa ya Songea   Chiyando   Muyenjwa Matoke kwa  tuhuma  za  matumizi  mabaya ya  nyaraka    kwa lengo  la kumdanganya  mwajiri na  kujipatia  fedha  kiasi cha  zaidi ya  shilingi  milioni  64.
Watuhumiwa  hao  walifikishwa  jana  kizimbani  mbele ya  Hakimu  Mkazi  wa  Mahakama  ya  Wilaya ya  Mpanda   Chiganga  Ntengwa  na  kusomewa  mashitaka  na  wanasheria wa   TAKUKURU wa  Mkoa  wa  Katavi   Bahati  Haule  na  Simon  Buchwa  .
 Watuhumiwa hao  ambao wote watatu walikuwa wakitetewa  na  mwanasheria  Elias  Kifunda  wanadaiwa  kutenda kosa  hilo kinyume  cha  sheria  cha kifungu  cha 22 cha  sheria  ya kuzuia  na kupambana  na  Rushwa    namba  11 ya  mwaka  2007.
Wanasheria wa  TAKUKURU walidai  kuwa  watuhumiwa  hao  walitenda  kosa  hilo  hapo   Januari   2 mwaka  2012 wakishirikiana  na wakandarasi waliokuwa wakitengeneza  barabara ya kutoka  Nsemlwa  ,Kasokola  hadi  Mtapenda  na  kutengeneza nyaraka za malipo ya kiasi cha  shilingi  milioni   64, 376,152
 Washitaka  hao wanadaiwa  kutenda  kosa  hilo wakati wakiwa ni  watumishi wa  Halmashauri ya  Wilaya ya  Mpanda   ambapo mshitakiwa wa  kwanza Godfrey  Majuto wakati  huo alikuwa ni  Mwandisi  wa  ujenzi   na  mshitakiwa wa pili  Naomi  Ndelilio  Nnko  alikuwa  ni  kaimu  Mkugenzi  wa  Halmashauri  ya  Wilaya ya  Mpanda   ambapo kwa   sasa  ni  mkurugenzi wa  Halmashauri ya  Wilaya ya  Serengeti na  Majuto kwa sasa ni  mwandisi wa Manspaa ya  Songea.
Wanasheria  hao wa kutoka  TAKUKURU waliendelia  kuiambia   mahakama  kuwa watuhumiwa  hao watatu walishirikiana  kutenda  kosa hilo wakiwa  na  watuhumiwa  wengine  wawili  ambao hawakuweza kufikishwa  mahakamani  hapo  jana  ambao waliwataja  kuwa ni   Petro  Mwanoni  na   Beatus Bisesa ambao  nao wanatarajiwa kufikishwa  mahakamani wakati wowote.
Baada ya  kusomewa  mashita hayo  watuhumiwa  wote  watatu  walikana   mashitaka  hayo na  walipewa  mashariti ya  mdhamana  ambapo kila  mmoja  alitakiwa kudhaminiwa kwa kiasi cha   shilingi  milioni  kumi  keshi  hau  mali  ambayo  haihamishiki  na  hati zao za  kusafiria kuzikadhisha  mahakamani
Hata  hivyo  watuhumiwa   wawili  Majuto   na   Nnko waliweza kutimiza  masharti  na  kupewa  mdhama ina  mshitakiwa   Chiyando   Muyenjwa   Matoke  alishindwa  kutimiza  mashariki ya  mdhamana na kupelekwa  rumande.
Hakimu   Mkazi   mfawidhi  Chiganga  Ntengwa aliihairisha  kesi hiyo   hadi  hapo   Mei   28  mwaka huu  kwa  ajiri ya  kupangiwa  tarehe ya kuanza kusikilizwa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa