Home » » POLISI KATAVI WAKAMATA WATU 2 WAKIWA NA RISASI 70 ZA SMG NA SAR

POLISI KATAVI WAKAMATA WATU 2 WAKIWA NA RISASI 70 ZA SMG NA SAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

           Na  Walter  Mguluchuma
                Kataviyetu blog
 Watu  wawili wakazi wa Mtaa wa  wa  Mji wa  Zamani  Manspaa ya  Mpanda  wanashikiliwa  na  Jeshi  la  Polisi  Mkoa wa  Katavi  kwa tuhuma  za kukamatwa wakiwa na  Risasi     70  za  Bunduki aina  ya SAR  na  SMG wakiwa wamezihifadhi  ndani ya  Kopo  la oil.
Watuhumiwa  hao  ambao  majina  yao  yamehifadhiwa kwa  kuwa upelelezi  bado  unaendelea  walikamatwa  hapo  juzi   majira ya saa kumi  na  moja  na  nusu  jioni  huko  katika   Mtaa wa  Mji wa  zamani   mjini  hapa .
Kaimu Kamanda wa  Polisi wa  Mkoa  wa  Katavi   Damas   Nyanda  aliwaambia  waandishi  wa  habari jana  ofisini  kwake  kuwa  watuhumiwa  hao walikamatwa kufuatia  jeshi la  polisi  kupata  taarifa za kutoka  kwa  Raia  wema kuwa watu hao wanamilki  Risasi  kinyume  cha  sheria .
 Alisema  baada ya Polisi  kupata  taarifa  hizo  walianza kufanya  uchunguzi na  ndipo  siku  hiyo ya juzi walipofanikiwa  kuwakamata  watuhumiwa wakiwa na  Risasi  70 za  bunduki aina ya  SAR  na      SMG  wakiwa  wamezihifadhi ndani ya  nyumba yao  zikiwe  kwenye  kopo la  OIL lenye  rangi  ya kijivu.
Wakati huo  huo  jeshi la  polisi  Wilayani  Mpanda  linawashikilia  watu wawili wakazi wa   Mji wa  zamani  kwa tuhuma  za kuwakamata wakiwa na  Bhangi   kete  705 na  debe  mbili za  Bhangi wakiwa  wamezififadhi   ndani ya nyumba wanayoishi.
Kaimu  Kamanda  wa  Polisi wa  Mkoa  wa  Katavi  Damas  Nyanda  alisema  watuhumiwa  hao  wawili  ambao  majina  yao  bado  yamehifadhi  na jeshi   hilo  walikamatwa hapo  juzi  majira ya  saa  kumi na  mbili  jioni  huko   katika   Mtaa wa  Mji wa  zamani .
 Alieleza  mbele  ya  waandishi wa  Habari  kuwa watuhumiwa  walikuwa wameihifadhi  Bhangi  hiyo  ndani ya  mifuko ya   sandarusi  huku  wakiwa wameificha  ndani  ya  nyumba yao  wanayoishi .
Kaimu  Kamanda  Nyanda  alisema  watuhumiwa  wa  matukio hayo  yote  mawili  bado wanashikiliwa na  jeshi  la  Polisi  na  wanatarajiwa kufikishwa  Mahakamani  baada ya  uchunguzi wa matukio  haya utakapo  kuwa  umekamilika ili wakajibu  Washita Mahakamani  yanayowabili .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa