Home » » HATARI HII: WATU WATATU WAKAMATWA WAKIWA NA KADI 19 ZA ATM WAKITOA FEDHA TAWI LA NMB

HATARI HII: WATU WATATU WAKAMATWA WAKIWA NA KADI 19 ZA ATM WAKITOA FEDHA TAWI LA NMB

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na    Walter  Mgulucuma
      Katavi Yetu Blog
  Jeshi la  Polisi  Mkoa wa  Katavi linawashikilia  watu watatu   kwa tuhuma za  kukamatwa   wakiwa wanatoa   fedha   Tawi la  NMB       Mpanda kiasi  cha  shilingi  milioni 3,680.000  wakiwa  na  kadi  za  ATM  19   mali  za watu  tofauti   pamoja  na   Namba  za siri  za  kadi  hizo .
  Kaimu   Kamanda    wa  Polisi  wa  Polisi wa  Mkoa wa   Katavi     Damasi  Nyanda   aliwaambia   Waandisi wa  Habari  kuwa watuumiwa  hao watatu walikamatwa  hapo  jana   majira ya saa  tatu  usiku  katika  Tawi  la  NMB   Mpanda .
   watuhumiwa  hao  ambao  majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa  umepelelezi  bado  unaendelea  walikamatwa  na  Askari wa  Jeshi la  polisi  waliokuwa wakilinda  Benki    hiyo.
  Nyanda  alieleza  watumiwa  walikamatwa  baada ya  Askari  polisi  kuwatilia  mashaka   kutokana  na  kuwaona  wakiwa  wamekaa  muda  mrefu   kwenye   chumba   cha  mashine  ya kutolea  feda .
  Baada ya  kuwatilia  mashaka  polisi  waliingia  ndani ya  chumba  hicho na  kuwakuta watumiwa    hao wakiwa  wanaendelea  kutowa  fedha   katika  mashine  tatu   zilizomo  kwenye   mashine  za  kutolea  fedha .
Kaimu   Kamanda   alieleza  ndipo  Askari  polisi  walipoamua kuwapekua watuumiwa   na  waliweza kuwakuta  wakiwa  na   kadi  za  ATM  19 mali za watu  tofauti   pamoja  na   Namba  za   siri   za  kadi  izo  na  walikuwa  tayari  wameisha  towa  kiasi  cha  fedha   tasilimu   silingi  milioni    3,680,000.
 Alizitaja  Namba  za  Kadi za  ATM  walizokamatwa  nazo  watuumiwa  kuwa  AC 61908000058,AC 61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC 61902240100,AC 61908000237,AC 61902400518 AC 61910000645, AC 61910004240,AC 61908000609  AC 61902403168.
  Kaimu  kamanda  Nyanda  alizitaja  kadi  za  ATM  nyingine  zilizokamatwa   kuwa   ni zenye   namba  AC   61910000537,AC 61902402653, AC   61910000250, Ac   61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC     61910002329  na  AC , 70408100131.
Alisema  watuhumiwa  wanatarajia  kufikishwa  mahakamani   baada  ya  uchunguzi wa tukio  hili utakapokuwa umekamilika  na  bado watuumiwa  wote  watatu wanaendelea kushikiliwa na  jeshi la  polisi kwa mahojiano  zaidi .
  Kaimu  kamanda  ametowa  wito kwa wananchi  kuacha  tabia ya  kutowa  siri kwa watu za   namba  zao  za  siri  za  kadi wanazozitumia za  ATM   za  kwenye    Mabenki .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa