Home » » CWT MPANDA WATOA DARASA KWA VIONGOZI WANAWAKE SEHEMU YA KAZI

CWT MPANDA WATOA DARASA KWA VIONGOZI WANAWAKE SEHEMU YA KAZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


  Na  Walter  Mguluchuma
  Katavi yetu blog
   Chama  cha  Waalimu   CWT  Wilaya ya  Mpanda    kimetowa mafunzo kwa waalimu   Viongozi   Wanawake   katika  sehemu ya   kazi  mafunzo yakuwafanya Waalimu  Wanawake  wafahamu haki  zao na kuzilinda  na ujasiliamali
Mafunzo  hayo ya  siku moja  yalifanyika  jana  katika  ukumbi wa Kanisa   Katoliki  Jimbo la Mpanda  na kufunguliwa  na  Mwenyekiti wa  CWT  Wilaya  ya  Mpanda  Jumanne  Msomba.
 Katika  hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo  hayo  Msomba  alieleza kuwa  Waalimu Wanawake  wamekuwa wakikabiliwa na  changamoto  mbalilmali  ambazo  wamekuwa wakishindwa kuzipatia ufumbuzi kutokana na  kutofahamu  haki zao  zinazo walinda.
 Alisema   ndio  maana CWT   kitengo cha Wanawake  imeona  umuhimu  wa kuwapatia  mafunzo hayo ya siku moja   yenye  lengo  la kuwafundisha  watambue  haki zao na sheria za utumishi pamoja na ujasilmali  ili waweze kujiongezea kipato chao .
Mwenyekiti  huyo  aliwataka  Waalimu  kufanya  kazi  kwa kufuata  taratibu za kazi  katika utumishi wao  kwa   kufanya kazi  kwa bidii na kwa kujituma  iliweweze  kutekeleza vizuri majukumu ya kazi yao  za kila  siku .
 Pia  wawe karibu na  chama chao cha Waalimu na  wawe ushirikiano na pindi  mwalimu mwanamke  anapokuwa amepata matatizo sehemu ya kazi apelike  mapema  taarifa CWT .
Nae  Kaimu  Katibu wa CWT Wilaya ya Mpanda   Masanja  Manyanga  alisema  Kitengo cha wanawake cha   CWT  kinalojukumu  la  kuwakumbusha  walimu wanawake  majukumu  yao .
  PIa aliwataka waalimu wa  Wanawake   waweze kujitambua  kwa kuvaa  mavazi yenye  heshima na   wewe  na  lugha  nzuri  kwa jamii inayowazunguka  pamoja na  kuwa na tabia ya kuwashauri wanafunzi wa kike pindi wanapoona  mwenendo wao unapokuwa umeanza kubadilika  kimaadili .
  Manyanga alisema   chama cha Waalimu  kimeamua kuwapatia  mafunzo waalimu  wanawake ya ujasiliamali   ili waweze  kujitambua  na waweze kujipatia kipata  kitakachowafanya watoke   kwenye uchumi  dhaifu .
 Alisema  bado baadhi ya watu wanazoimani potofu  wanaamini  kuwa  mwanamke  hastahili  kumiliki mali  yoyote  jambo  ambalo sio  sahihi .
Mmoja wa  washiriki wa  mafunzo hayo  Mwalimu   Siyawezi   Machulo   alisema  wamekuwa wakikabiliwa  na  changamoto  mbalimbali wao  kama waalimu .
  Alitaja  baadhi ya  changamoto hizo kuwa ni  kutolipwa  fedha  za likizo kwa kipindi cha muda mrefu sasa na  kutorekebishiwa  mishahara kwa wakati pindi wanapokuwa wamepandishwa  daraja .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa