Home » » HATARI: AFA BAADA YA KUTOKEA UGOMVI WA KIGOMBEA VIROBA AINA YA ZED WAKIWA KATIKA SHEREHE YA KUTOA MTOTO NJE

HATARI: AFA BAADA YA KUTOKEA UGOMVI WA KIGOMBEA VIROBA AINA YA ZED WAKIWA KATIKA SHEREHE YA KUTOA MTOTO NJE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter   Mguluchuma 
Katavi 
Mkazi wa Mtaa wa  Mji wa  Zamani  Manispaa ya  Mpanda  Mkoa wa  Katavi    Shukuru  Korongo  32  amefariki  Dunia  baada ya kupigwa na  mwenzake baada ya kutokea ugomvi wa  kugombea  Viroba vya pombe  aina ya  zed wakati wa sherehe za kumtoa  nje mtoto wa jirani yao.

Mwenyekiti wa Mtaa huo  Magreti  John  Kitunguru  aliwaambia  waandishi wa habari jana  kuwa tukio  hilo  lilitokea  hapo  juzi  majira ya saa  tano  usiku  katika  mtaa huo wa  Mji wa  zamani .

Mwenyekiti huyo wa  mtaa alisema  siku  hiyo ya  tukio  marehemu  alikuwa   na  rafiki  yake  aitwaye  Pisikitu  Maiko wakiwa  nyumbani kwa jirani yao  ambae  alikuwa  amewaalika  katika  sherehe za  kumtoa  mtoto wake  nje.

  Alisema   ndipo   marehemu  alipopewa  viroba vya  Zed  na  mwandaaji wa sherehe  hizo ili aweze kuwagawia watu waliokuwepo kwenye  sherehe  hizo  za kumtoa  mtoto  nje .
Alieleza  ndipo   Pisikitu alipoanza kumtuhumu  marehemu kuwa viroba  alivyowagawia ni vichache  hivyo  alimtaka  amwongezee  viroba  vingine kwani  alipewa vingi na  amevificha .

  Hata  hivyo  marehemu alikataa kata  kata kumwongezea   viroba  vingine kwa kile alichodai kuwa viroba  alivyobaki  navyo vinamtosha yeye mwenyewe  kuvinywa na kuvimaliza .

Mwenyekiti  huyo wa  mtaa alieleza  kuwa  ndupo baada ya  hapo ndipo ulianza ugomvi wa kupigana  baina ya  Marehemu na  Pisikiti  hadi hapo  marehemu alipozidiwa na kuanguka  chini  hari  ambayo ilipelekea wambebe  marehemu  hadi chumbani kwake na  ilipofika  majira ya saa 12 ya  arufajili mama  mzazi wa Shukuru  alimkuta   akiwa  ameisha  fariki  Dunia.

Ndipo  mama wa  marehemu alipotoa  taarifa kwa  uongozi wa  serikali ya  mtaa ambao walifika kwenye eneo hilo na  kasha walitowa taarifa kwa jeshi la  polisi  ambao walifika  kwenye  eneo hilo.

Kaimu  Kamanda wa  Polisi wa Mkoa wa Katavi  Damas  Nyanda  amethibitisha  kutokea kwa kifo  hicho  katika  mtaa wa  Mji wa  zamani  hapo  juzi na alisema mwili wa  marehemu upo katika  chumba cha kuhifadhi maiti  katika  hospitali ya  wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya uchunguzi wa kidaktari.

Na  Jeshi la  polisi  linamshikilia   Pasikiti  Maiko kwa  mahojiano zaidi  kuhusiana  na kifo  hicho  wakati jeshi hilo  likiwa  linaendelea  na  upelelezi zaidi .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa