Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Waziri Mkuu msitaafu Mizengo Pinda amesema kuwa Watanzania wanayoimani kwamba Taasisi ya Benjamini Mkapa itaendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Serikali ya awamu ya tano ya Mhe Dkt John Magufuli ambae ameonyesha dhahiri kuuguswa na suala la kuimarisha afya ya Watanzania.
Pinda alitowa kauli hiyo katika sherehe ya makabidhiano ya nyumba 19 za watumishi wa afya zilizotolewa na Taasisi hiyo kwa ajiri ya Mikoa ya Katavi na Rukwa zilizofanyika juzi katika Zahanati ya Kabungu Wilayani Mpanda ambapo alikuwa mgeni rasmi wa sherehe hizo .
Alisema Taasisi ya Benjamini Wiliam Mkapa maarufu Mkapa Foundation imeweza kuratibu na kuwezesha kupatikana kwa msaada huo mkubwa uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni.
Pinda alieleza Serikali yetu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya kwa nia ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya kwa nia ya kuimarisha afya za wananchi wake ,mikakati na jitihada za makusudi zimeendelea kutekelezwa katika kuimarisha utoaji wa huduma za utoaji wa huduma za afya husani maeneo ya Vijijini.
Licha ya mafanikio yaliyopatikana Nchi yetu bado inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa watumishi wa afya hasa maeneo ya Vijijini nay ale yasiyofikika kwa urahisi upungufu wa watumishi wa afya unakadiliwa kuwa zaidi ya asilimia 50 ya mahitaji katika vituo vyote vya kutolea huduma ya afya nchini.
Alisema anafarijika kuona leo hii katika kuimarisha huduma za afya Wizara ya afya,Maendeleo ya jamii , Wazee na watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamini Wiliam Mkapa zimesaidia Mikoa ya Katavi na Rukwa katika kuhakikisha malengo ya Kitalfa upatikanaji wa watumishi wa afya wa kutosha na wenye sifa yanafikiwa kwa haraka.
Pinda alieleza kuwa ukizingatia huu ni wakati wa kutekeleza kaulimbiu ya Hapa kazi Tu basi anatumia furusa hiyo kwa Halmashauri kuhakikisha zinaweka fedha za kutosha na utaratibu kulingana na miongozo kuhusu ukarabati wa majengo zikiwemo pia nyumba za watumishi iliwaishi katika mazingira mazuri na waweze kutoa huduma bara na stahiki kwa wananchi.
Nae afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Benjamin Wiliam Mkapa DKT Ellen Senkoro alieza ujenzi wa nyumba hizo 19 walizokabidhi umegharimu jumla ya shilingi Bilioni 1,394,093,806 ambapo wastani wa nyumba moja umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 73.3.
Alisema Taasisi hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2006 mpaka sasa imeisha jenga nyumba 480 kati Halmashauri 51 nchini na miongoni mwa nyumba hizo nyumba 30 zimejengwa katika Mikoa ya Katavi
na Rukwa.
Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt Naibu Mkongwa alisema ujenzi wa nyumba hizo utasaidia kupunguza adha kwa wananchi ambao walikuwa wakikosa huduma kwa muda usiku kutokana na waganga na wauguzi kuishi mbali na zahanati kwa kuwepo kwa nyumba kutafanya huduma zipatikane muda wote kwenye vituo ambavyo Taasisi imejenga nyumba .
Muuguzi wa Zahanati ya Kabungu Rose Mpimbe alieleza kupatikana kwa nyumba ya kuishi katika Zahanati kutamwondolea tatizo la kutembea umbali mrefu kwani allikuwa akiishi kijiji cha jirani kilichopo umbali wa kilimeta mbili kutoka kwenye Zahanati .
Alisema alikuwa analazimika kuaachwa usiku pindi kunapokuwa na mgonjwa na kulazika kutembea kwa miguu umbali huo mida ya usiku kwa ajiri ya kumuudumia mgonjwa ,
Mkazi wa Kijiji cha Kabungu Frida Futakamba alisema kukamilika kwa nyumba hiyo kutasaidia kupatikana muda wote huduma ya uzazi
kwa akina mama kwani wajawazito walikuwa wanalazimika kutafuta wakunga
wa jadi kwa ajiri ya kuwasaidia kujifungua kutokana na zahanati yao kutokuwa na huduma mida ya usiku kutokana na wataalamu kuishi mbali na Zahanati .

0 comments:
Post a Comment