Home » » HATARI: WANANDOA WANUSURIKA KIFO BAADA YA KUMUA MTOTO WAO WA MIAKA 3 KWA KUMCHOMA NA MOTO NA KUUFICHA MWILI WA MAREHEMU NDANI YA CHUMBA

HATARI: WANANDOA WANUSURIKA KIFO BAADA YA KUMUA MTOTO WAO WA MIAKA 3 KWA KUMCHOMA NA MOTO NA KUUFICHA MWILI WA MAREHEMU NDANI YA CHUMBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


   Na  Walter  Mguluchuma
     Katavi  yetu blog
Wanandoa wawili Juma  Selemani  (28     na  Suzana  Elias  24 wakazi wa Mtaa wa mji wa zamani Manispaa ya Mpanda wamesurika kifo kutoka kwa kundi la wananchi waliotaka kuwauwa kwa kuchoma  motonyumba waliokuwa wakiishi  baada ya kukasirishwa na kitendo chao cha kumua mtoto wao aliyejulikana kwa jina la  Justina Laulenti (3(  kwa kumchoma na moto kichwani na mikononi na kasha kuuficha mwili wa marehemu ndani ya chumba walichokuwa wakiishi kwa muda wa siku tatu.
Tukio hilo la kusikitisha la mauwaji ya mtoto huyo lilitokea hapo jana  majira ya saa moja na nusu usiku katika mtaa huo wa mji wa zamani mjini hapa na lilisikitisha watu wengi  wa Manspaa ya mji wa Mpanda
Mwenyekiti wa Mtaa huo Magreti  John( Mhaya alimweleza mwandishi wa gazeti hili aliyekuwepo kwenye eneo hilo la tukio  kuwa alipata taarifa  za  kuuawa  kwa mtoto huyo  ambae alikuwa akiishi na baba wake wa kambo  aliyekuwa amemuowa mama yake Suzana  Elias.
 Alisema  baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa  wangaji wa nyumba hiyo alifika kwenye nyumba hiyo na ndipo walipomweleza kuwa kuna mtoto ameuawa na wazazi wake  na wamemfungia ndani  wakiwa wameuficha mwili huo wa marehemu kwa muda wa siku tatu .
Mwenyekiti huyo wa mtaa alieleza  wapangaji hao walishitushwa  baada ya kuona mtoto huyo  kutoonekana kwake  kwa muda wa siku  tatu na chumba walichokuwa wakiishi wanandoa hao  kuanza kutowa harufu ya kitu kilicho oza na  kila walipoulizwa  mtoto wao yuko wapi  walionekana wanandoa hao kuwa na mashaka na walijibu kuwa mtoto wao  anaumwa.
Ndipo walipoamua  kutowa taarifa kwa mjumbe wa serikali ya mtaa anaeitwa  Matha Idd ambae nae alitowa taarifa kwa kwake yeye  Mwenyekiti wa mtaa  ambae aliwapatia tarifa  jeshi la Polisi na waandishi wa Habari .
Polisi walifika kwenye eneo hilo na kukuta kundi la watu huku wakiwa na silaha za jadi  mawe na fimbo  wakiwa  wameizingira nyumba hiyo kwa lengo la kutaka kuwashambulia wanandoa wengine huku wengine wakiwa wamshika mafuta ya taa kwa lengo la kutaka kuchoma nyumba hiyo .
  Askari polisi ambao walikuwa na silaha za moto walifanikiwa  kuwatawanya wananchi hao na kasha waliingia ndani ya chumba  na kuwachukua wanandoa hao wawili na kuwapeleka  kituo cha polisi cha Mpanda mjini huku wananchi hao wakiwasindikiza kwa kuwarushia  mawe.
Kisha polisi waliokuwa wamebaki hapo pamoja na mwenyekiti wa mtaa walifnya uchunguzi wa awali wa kuukagua mwili wa marehemu mtoto huyo na waliweza kuukuta ukiwa  umechomwa na moto  kichwani na mikononi  huku ukiwa umeanza kuharibika na ukiwa unatowa maji mwilini.
Mmoja wa wanandoa hao aliyejitambulisha kwa jina la Maria Komba alieleza kuwa kabla ya tukio hilo  amekuwa akisulisha ugomvi wa mara kwa mara  ambapo  Juma Selemani alikuwa akipinga kitendo cha mke wake kuishi nyumbani kwake marehemu na alikuwa akimtaka mkewe ampeleke kwa baba yake mzazi kwani yeye alikuwa akidai hawezi kukaa na kumtunza mtoto ambae sio wake .
Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi wa Mkoa wa Katavi Mohamed Rashid I amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikisha .
Alisema  wanandoa hao wote wawili wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi  utakapo kuwa umekamilika 


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa