Home » » HATARI: AUAWA KWA KUCHOMWA NA KISU BAADA YA KUFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MKE WA MTU

HATARI: AUAWA KWA KUCHOMWA NA KISU BAADA YA KUFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MKE WA MTU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog

Mtu mmoja  aliiyejulikana kwa jina la  Gidison  Visent 32 Mkazi wa Kijiji cha Katuma Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda ameuawa kwa kuchomwa na kisu kifuani na Mohamed Muna  Mratibu wa Elimu wa Kata ya Katuma baada ya kumkuta akifanya mapenzi na mke wake ndani ya chumba  chake cha kulala.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa tukio hilo lilitokea hapo  juzi mida ya saambili na nusu katika Kijiji hicho cha Katuma nyumbani kwa mtuhumiwa Muna.

Siku hiyo ya tukio mtuhumiwa  alimkuta  marehemu  akiwa  ndani ya nyumba yake chumbani  huku akiwa  anafanya mapenzi  tendo la ndoa  na mke wake anaitwa Ester Kasansa 36.

 Alisema kitendo hicho cha kumfumania mkewe akiwa anafanya mapenzi   na marehemu kilimkasirisha mtuhumiwa na ndipo alipoamua  kumchoma  kisu  marehemu  na kufariki Dunia hapo hapo na kasha alikimbia.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa