Home » » AFA BAADA YA KUPIGWA KWA KUKUTWA ANAOGEA NA DADA WA MTUHUMIWA

AFA BAADA YA KUPIGWA KWA KUKUTWA ANAOGEA NA DADA WA MTUHUMIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Katavi
Mkazi wa  Kijiji cha Kalovya Tarafa ya Inyonga Wilaya ya  Mele Ramadhani  Ally (26) amefariki Dunia  wakati akiwa  anapatiwa matibabu  kufuatia  kipigo kikali  alichokipata  kutoka kwa  Ntemwa  Kabembanya(26) Mkazi wa Kijiji cha Ipwaga Tarafa ya Inyonga  baada ya kukutwa barabarani akiwa  anaongea na dada wa mtuhumiwa  wa tukio hilo.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa  Habari tukio hilo lilitokea  hapo juzi majira ya saa kumi na mbili na nusu  katika Kijiji cha Ipwaga.
Siku hiyo ya tukio    mtuhumiwa  Ntemwa  alimkuta marehemu  akiwa amesimana dada yake aitwaye  Ngoro  Mbogo (12) huku wakiwa wanaongea .
 Kamanda Kidavashari aliwaambia Waandishi wa Habari  kitendo hicho  cha  kuwakuta wakiwa wamesimama huku wakiwa wanaongea kirimkasirisha sana Mtuhumiwa .
Ndipo pasipo kumwambia neno lolote  alianza kumshambulia kwa kupiga  na fimbo  katika sehemu mbalimbali za mwili wake  huku dada wa mtuhumiwa akiwa anashuhudia kipigo hicho.
Alisema  mtuhumiwa aliendelea kumshambulia  na marehemu alipoona kipigo kimzidia alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani  ambao walifika kwenye eneo hilo na kumkuta marehemu akiwa hoi .
 Na walimchukua na  kumpeleka  katika Hospitali ya Wilaya ya Mlele kwa ajiri ya kupatiwa matibabu na alipofikishwa hapo alilazwa wodini kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Kamanda Kidavashari alisema wakati akiwa anaendelea kupatiwa matibabu  kwenye Hospitali hiyo  alifariki Dunia  .
 Alieleza   kuwa Jeshi la Polisi  linamshikilia   mtuhumiwa Ntemwa  Kabembanya   na  anatarajiwa  kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika ili  akajibu tuhuma inayo mkabili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa