Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia
watu wawili kwa tuhuma za kumshambulia
kwa kumpiga na kumjeruhi Jeneroza Roba (60) Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa Mjini Mpanda baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana
kuwa tukio la kupigwa na kushambuliwa
kwa mwamke huyo lilitokea hapo juzi majira ya saa tano asubuhi katika mtaa wa
Mji wa Zamani mjini hapo.
Kidavashari
aliwataja waliokamatwa na Polisi kuwa
ni Ashura Msaguzi (30) Mkazi wa Mji wa Zamani ambae ni
mtumishi wa chuo cha maendeleo ya jamii cha Msaginya Mkoani hapa na Aisha Sungura (28) Mkazi wa mtaa wa mji wa
Zamani.
Alisema siku hiyo ya tukioj Jeneroza alikuwa akipita kwenye
mtaa wa mji wa Zamani akiwa anaelekea
nyumbani kwake katika Mtaa wa Nsemlwa
Ndipo mtuhumiwa Ashura alipomwona Jeneroza na kuanza
kupandisha mashetani huku akiwa anamtaja
Jeneroza kuwa ndie aliyemloga .
Kitendo hicho cha
kupandisha mashetani kilimshawishi Aisha
kuungangana na Ashura na
kisha walianza kumshambulia kwa kumpiga Jeneroza na
kisha walimvua nguo na kumwingiza ndani ya nyumba hiyo
Alisema kitendo hicho kiliwakasirisha watu
walioshudia hari ambayo iliwafanya wananchi
waanze kuishambulia kwa mawe nyumba hiyo kwa lengo la kumwokoa Jeneroza ambae
alikuwa amefungiwa ndani ya nyumba ya
wazazi wake na Ashura.
Kidavashari
alieleza Mwenyekiti wa Mtaa huo Magreti
John(Mhaya) alifika kwenye eneo hilo na baada ya kuona hari ya
wananchi ya kuishambulia nyumba
hiyo kwa mawe ikiwa inazidi kuongezeka alitowa taarifa kwa jeshi la Polisi .
Polisi baada ya
kufika kwenye eneo hilo waliweza kuwatawanya wananchi hao na waliweza kufanikiwa kumtowaNdani ya nyumba
Jenaroza na kuwakamata watuhumiwa
na kuwafikisha katika kituo cha Polisi
cha Mpanda .
Kamanda
Kidavashari alisema watuhuwa bado wanaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na
mara upelelezi utakapo kamilika
wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani
ili wakaji mashika yanayo wakabili.
Amewataka wananchi
wa Mkoa wa Katavi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikoni pindi panapo kuwa pametokea migogoro ya ya maswala ya kijamii na badala yake waende
kwenye vyombo vya sheria.
0 comments:
Post a Comment