Home » » VIONGOZI WA SERIKALI ,DINI NA SIASA WATAKIWA KUELIMISHA WATU UZAZI WA MPANGO

VIONGOZI WA SERIKALI ,DINI NA SIASA WATAKIWA KUELIMISHA WATU UZAZI WA MPANGO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mgombea  Ubunge  wa Jimbo la Nsimbo   Wilayani  Mlele  Mkoa wa Katavi Elias Kifunda (ACT WAZALENDO TANZANIA) amewataka viongozi wa Serikali  wadini na wavyama vya siasa kuwaelimisha watu umuhimu wa uzazi wa mpango
Kifunda ambae  ni Wakili wa kujitegemea aliyasema hayo hapo jana ofisini kwake  katika  eneo la madukani  mjini  Mpanda wakati akizungumza na mwandishi wa gazeti hili
Alisema  kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu hapa Nchini  za zaidi ya nusu ya watu hao  ni wale ambao  wanaumri  mdogo   na  matokeo yake  Serikali imekuwa ikibeba mzigo mkubwa wa kuwaudumia watu  kwa kuwa ni jukumu la Serikali kuhudumia watu
 Alifafanua kuwa  idadi ya watu  ni lazima  ilingane  na uwezo  wa Serikali  wa kuwahudumia watu  wake katika maswala  mbalimbali  kama vile Elimu  Afya Maji  na huduma nyinginezo
 Alisema  uzazi wa mpango  ni swala muhimu sana  ingawa  swala hilo lilikuwa  halijawekwa  mkazo  kitachotakiwa sasa  hivi  ni  watu  kupewa elimu ya madhara ya kuzaa  bila   mpangilio  na itolewe  mashuleni kwenye  vyuo na  katika  vituo vya afya na zahanati
 Hivyo  viongozi  wote wa Serikali Dini  na  vyama  vya siasa  wanalo jukumu  la kuelimisha watu  umuhimu wa uzazi wa mpango  na  ndio maana zipo baadhi ya nchi zimetunga   sheria  za idadi  ya watu   ambao mtu anatakiwa kuzaa
 Alisema  uzazi  wa mpango  unasaidia  mtu  kuzaa watoto  ambao  anakuwa  na uwezo  nao  wa kuwahudumia  mahitaji  ya lazima ya binadamu
 Kifunda  alisema  watoto wachanga  ni kundi  ambalo  wanaathilika  zaidi na   maradhi  kwani watoto wachanga  hawezi  kujihimili  wenyewe hivyo  endapo atachaguliwa  kuwa  Mbunge   ataakikisha huduma  za   mama  na  watoto  wachanga zinaimarika katika jimbo lake na Taifa kwa ujumla

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa