Home » » HATARI: JESHI LA POLISI MPANDA LALAZIMIKA KUPIGA RISASI HEWANI KUWATAWANYA WAFUASI WA CHADEMA NA CCM KUTOKANA NA VURUGU KUBWA ILIYOTOKEA ENEO LA SOKO KUU.

HATARI: JESHI LA POLISI MPANDA LALAZIMIKA KUPIGA RISASI HEWANI KUWATAWANYA WAFUASI WA CHADEMA NA CCM KUTOKANA NA VURUGU KUBWA ILIYOTOKEA ENEO LA SOKO KUU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
JESHI  la Polisi  wilayani Mpanda  katika mkoa wa Katavi wamelazimika  kupiga  risasi hewani  ili kuwatawanya  wafuasi  wa CCM na Chadema  kufuatia  vurugu kubwa  iliyotokea  eneo la Soko Kuu  mjini hapa  jana  na kusababisha wafanya biashara  wafunge  maduka yao .
Vurugu hiyo  ilisababishwa na  wafuasi  hao wa Chadema na CCM  kugombania  “kijiwe”  kimoja  kilichopo  eneo la Soko Kuu mjini hapa  kutundika  bendera za  vyama vyao  vya saisa  na mabango ya wagombea wao .

Mkasa huo ulitokea  saa moja na nusu  usiku  katika eneo la Soko Kuu  mjini Mpanda  katika Mtaa wa Kashaulili baada ya wafuasi wa CCM wakiongozana na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kashaulili , Mage Kitunguru ( “Mhaya” ) kufika kwenye kijiwe  hicho  wakiwa na bendera za CCM  na mabango ya wagombea wao  wakitaka kutundika .
Kwa mujibu wa mashuhuda  walikuwa katika eneo  hilo  wanaeleza kuwa kitendo  hicho  cha wafuasi  hao  wa CCM  na mwenyekiti wao wa Mtaa  kutaka  kutundika  bendera  za CCM katika kijiwe cha kiliwasirisha sana  wakiwadai kuwa  kijiwe hicho  ni mali  ya Ukawa  hivyo CCM  hawastahili  kutundika  bendera zao  wala kupandika  mabango  ya wagombea wao .
“ Wafiasi wa vyama  hivyo  viwili  vya siasa walianza kurushiana maneno makali  wakitishiana  maisha  huku wakizomeana .... hali  iliyosababisha umati  wa watu  kukusanyika katika eneo hilo  na kuhatarisha uvunjifu wa  amani na utulivu wa eneo hilo “ alisema mtoa taarifa  kwa masharti ya kutoandikwa jina lake .
Askari polisi  wakiwa na silaha  walifika  katika eneo hilo la tukio  lakini  walipojaribu  kuwatuliza  wafuasi  wenye hasira  wa CCM na Chadema  kwa  amani waliendelea kulumbana na kutishiana  maisha .
Inadaiwa kuwa  ndipo  askari polisi  hao  walipolazimika  kufyatua  risasi hewani  ili kuwatawanya  wafuasi  hao  ambao  walitimua mbio wakitoka  eneo  hilo  la tukio .
“Polisi walipoaanza kufyatua risasi  hewani  wafanyabiashara walifunga  maduka yao  pia wauza matunda na mboga mboga  waliokuwa wakifanya  biashara  zao jirani  na eneo  hilo  la tukio  walilazimika kutimua mbio wakihofia usalama wa maisha yao “ alisema  mkazi wa Mtaa wa kashaulili aliyejitambulisha kwa jina  la Adam Michael
Ofisa wa Jeshi la Polisi kwa masharti ya kutoandikwa gazeti kwa kuwa si msemaji amekiri kutokea kwa tukio  hilo  akisisitiza kuwa  hakuna  maafa yeyote yaliyotokea kwamba jeshi hilo lilifanikiwa kumkatamata mtu moja  aliyejulikana kwa jina moja la Elick  Mkazi wa Mtaa w Majengo  Mjini hapa
Katibu wa CHADEMA wa Mkoa wa Katavi  Almasi Ntije alisema kuwa  Chama chake kimesikitishwa na kitendo kilichofanywa na wafuasi wa CCM cha kutaka   kuweka bendera na mabango ya wagombea wao kwenye jiwe cha wafuasi wa CHADEMA(UKAWA)
Alisema tume ya uchaguzi imeisha towa maelekezo kwa vyama vyote kufanya  shughuli zao mwisho ni saa kumi na mbili jioni  hivyo ameshangazwa na kitendo hicho  kufanywa na wafuasi wa CCM majira ya saa moja na nusu huku wakijua ni kinyume cha kanuni za tume ya uchaguzi
Nae  Mwenyekiti wa CCM wa  Wilaya ya Mpanda  Beda Katani  alikili  kuwepo kwa vulugu hizo za wafuasi  wa  vyama hivyo
Alisema  anasubiri apewa taarifa   nzima ju ya tukio hilo   ndipo atakapokuwa tayari kuzungumzia tukio hilo kama Mwenyekiti wa Chama

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa