Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi
wakiwa na silaha ya Kivita aina ya SAR
wamevamia Kitongoji cha Ruhafe Kijiji cha Vikonge Wilaya ya Mpanda Mkoa hapa na kuwapora wafanya biashara wa maduka kumi
na mbili vitu mbalimbali baada ya kufyatua risasi hewani ya kuwatishia
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari kuwa
tukio hilo la unyang’annnnnyi wa kutumia
silaha lilitokea hapo jana majira ya saa mbili na robo usiku katika Kitongoji
hicho cha Ruhafe
Katika tukio hilo majambazi hao walivamia
maduka 12 ya wafanyabiashara baada ya
kuwatisha kwa kufyatua Risasi hewani kwa kutumia bunduki ya kivita aina ya SAR
Majambazi hao
waliweza kupora vitu mbalimbali vikimemo
simu , Soral panal ,lap top ,
bidhaa za dukani na kisha baada ya kupola waliendelea kuwafyatua Risasi zisizo na idadi hewani
za kuwatisha wananchi wa eneo hilo na kisha walitokomea kusiko julikana
Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari kuwa
thamani ya vitu hivyo vyote vilivyopolwa bado
haijajulikana mpaka sasa
Alisema jeshi la Polisi kwa kwa kushirikiana na Wananchi na uongozi wa Kitongoji hicho walifanikiwa
kumkamata mtuhumiwa mmoja kuhusika na tukio hilo ambae alijulikana kwa jina la Yusuph
Malaki (35) Mkazi wa Makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mlele
Mtuhumiwa alikamatwa
akiwa na pikipiki moja aina ya
Sanlg yenye namba za
usajiri T.209 CEB Ambayo ilikuwa
ikitumiwa na majambazi hayo kwenye tukio hilo
Kamanda Kidavashari alisema juhudi
za kuwasaka watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo bado zinaendelea kwa polisi kwa kushirikiana na Wananchi
Mtuhumiwa
Yusuph Malaki bado anaendelea kushikiliwa na Polisi na
atafikishwa Mahakamani mara baada ya
uchunguzi wa tukio hili utakapo kuwa umekamilika
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment