Home » » HATARI: AUAWA KIKATILI KWA KUCHINJWA SHINGO

HATARI: AUAWA KIKATILI KWA KUCHINJWA SHINGO


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
 Mtu  mmoja aliyefahamika kwa jina la  Shija  Ngasa (35) Mkazi wa Kijiji cha  Katuma Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ameuwawa kikatili  kuchinjwa shingo  hadi kufa na watu wasio julikana  wakati akiwa na familia yake nyumbani kwake wakisubilia  kula chakula cha jioni 

Mauwaji hayo ya kutisha na yakikatili  yalitokea hapo juzi majira ya saa mbili   usiku nyumbani kwa marehemu  Shija   Ngasa katika Kijiji cha Katuma ambapo marehemu alikuwa akiishi na familia yake
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina msaidizi mwandamizi   aliwaambia jana waandishi wa Habari  kuwa  marehemu huyo  aliuwawa wakati  akiwa nyumbani kwake yeye na familia yake  wakati wakiwa wanasublia kula  chakula  cha  usiku kilichokuwa kinaandaliwa jikoni na mke wake
Alisema wakati wakiwa wanasubilia chakula  hicho ghafla walitokea watu wawili wasio fahamika  huku wakiwa  wamefunika uso wao  na mmoja wa watu hao alikuwa ameshika shoka mkononi
Aliwaeleza waandishi wa  Habari  kisha watu hao walimvamia  marehemu  na  kuanza  kumchinja kwa shoka  huku watoto wake  wawili wakiwa wanashuhudia  kitendo hicho cha mauwaji ya kikatili
Kidavashari  alisema  watoto   hao wa marehemu waliendelea kupiga mayowe ya  kuomba  msaada kwa majirani  na  ambao walifika kwenye eneo  hilo na kukuta watu hao wameisha tokomea  kusiko fahamika huku mwili wa marehemu ukiwa unagalagala  chini
 Alisema majirani walikwenda kutoa taarifa za    mauwaji hayo kwa viongozi wao wa Kijiji ambao  nao walitoa taarifa  kwa jeshi la Polisi Wilaya  ya Mpanda
Chanzo cha mauwaji   hayo ya kikatili   bado hakija julikana na mpaka sasa hakuna  mtu  wala watu waliokamatwa kuhusiana na mauwaji   hayo
Aidha jeshi la Polisi kwa kushirikiana  na uongozi  wa Kijiji hicho cha Katuma   wanaendelea  na jitihada  za kuwasaka na kuwabaini  na kuwakamata  wale  wote  waliohusika katika mauwaji hayo


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa