Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Waumini wa Kanisa
Katoliki Kigango cha Utende Porokia ya Inyonga Jimbo
Katoliki la Mpanda wamelazimika kushindwa kusali ibada ya misa ya sikukuu ya Pasaka kwa muda masaa
manne baada ya kutokea vulugu za kwaya
mbili za Kigango hicho kugombania kuimba
kwenye Ibada ya misa ya Pasaka na
kumtishia kupiga kwa mawe Katekisita wa
Kigango hicho
Tukio hilo
llitokea hapo juzi majira ya saa nne asubuhi ndani ya Kanisa la Kigango cha utende muda
mfupi baada ya kuanza kwa ibada ya misa ya sikukuu ya Pasaka iliyokuwa
ikiongozwa na Katekisita wa Kigango hicho Credo
Mwakipanda
Kwa mujibu wa
makamu mwenyekiti wa Kigango hicho Abel
Kalifumu alisema vurugu hizo
zilizihusisha kwaya mbili za Mtakatifi
Sesilia na Mtakatifu Agusino
Alisema uongozi wa Kigango hicho huwa wamaisha
zipangia utaratibu kwaya hizo wakati wa
sikukuu kuimba kwa zamu
kwenye misa moja
Alifafanua siku hiyo ya Pasaka wanakwaya wa
kwaya ya Mtakatifu Seselia walikataa wenzao wa kwaya ya Mtakatifu Agustino
wasiimbe kwenye ibada hiyo kwa kile walichodai kuwa siku hiyo ilikuwa ni zamu
yao kuimba peke yao
Alisema baada ya
mabishano ya muda mrefu wa kwaya hizo muda wa kuanza ibada ulifika na
Katekisita alipiga kengele kwa ajiri ya waumini ili waingie kanisani kwa kuanza
ibada ya misaa ya Pasaka
Wakati
Katekisita akiwa kwenye aktale kwa ajiri
kuendesha ibada ghafla kwaya hizo mbili kila mmoja alianza kiimba wimbo wake
kwa wakati mmoja hari ambayo ilipelekea kutokea hari ya kelele kubwa ndani ya kanisa hilo
Katikisa Credo
alizisihi kwaya hizo ziache vurugu
iliibada iendelee kama kawaida lakini wanakwaya wa Mtakatifu Sesilia
walimtishia Katekista kuwa endapo ataendelea na ibada watampiga kwa mawe
Kalifumu alieleza
baada ya katekista kuona hari ya vurugu imekuwa kubwa alilazimika kusitisha
ibada na kutoka nje ambapo alikuta hari ya vurugu ikiwa inaendelea na
ndipo alipovua kanzu yake na kuwakabidhi
viongozi wa kigango ambao walimsihi
arudi kanisani akaendelee na
ibada hata hivyo wanakwaya wa Mtakatifu Sesilia waliendelea kumtishia kuwa
akirudi kusalisha wanampiga mawe hari iliyomlazimu amue kweda kwake
Alisema
baada ya katekista kuwa amekwenda
nyumbani kwake viongozi wa kigango walimfuata
nyumbani kwake na kumsihi arudi lakini alikataa kata kata
Waumini wa Kanisa
hilo baada ya kuambiwa kuwa kateksta
amekataa kurudi waliteuwa wazee maarufu
wa kijiji hicho ambao waliongozana na
viongozi wa kigango hicho na kumsihi kateksta arudi kanisani na kuendesha ibada ombi ambalo katiksta Credo alikubali na
kurudi kanisani majira ya saa saba na nusu mchana
Alisema baada ya
kateksta kufika kanisani hapo aligonga kengele kwa ajili ya kuanza ibada ambapo
waumini wakanisa hilo waliziamuru kwaya hizo zisiimbe kwenye ibada hiyo na misa hiyo ilifanyika bila kwaya yoyote ile kuimba waumini waliimba
nyimbo za zamani
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment