Home » » HOT NEWS:MAKUBWA HAYA.. MGANGA WA JADI AKAMATWA NA FUVU LA KICHWA CHA BINADAMU

HOT NEWS:MAKUBWA HAYA.. MGANGA WA JADI AKAMATWA NA FUVU LA KICHWA CHA BINADAMU


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi  linamshikilia  mtu mmoja  Mganga maarufu  wa jadi kwa tuhuma za kumkamata akiwa na fuvu la kichwa cha Binadamu akiwa ameligifadhi ndani ya   choo  anachokitumia
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  aliwaambia waandishi wa habari  jana ofisini kwake kuwa  mtuhumiwa  Kabichi    Mhulu (39) Mkazi  wa Kijiji   cha Kakese Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  alikamatwa  hapo jana    majira ya saa kumi na mbili jioni nyumbani kwake  katika Kijiji  cha Kakese
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari   mtuhumiwa huyo alikamatwa na fuvu hilo la kichwa cha binadamu akiwa ame amelihifadhi  ndani ya choo alichokuwa akikitumia
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambae ni mganga maarufu wa kienyeji kulitokana na taarifa za  raia wema ambao waliokuwa wametowa taarifa kwa jeshi la polisi kuwa mganga huyo amehifadhi fuvu la kichwa ndani ya choo chake
 Alisema baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi la polisi  lilifika katika Kijiji  hicho cha Kakese na kisha walikwenda nyumbani kwa  mtuhumiwa kwa ajiri ya kumfanyia upekuzi
Kidavashari alieleza  Polisi walifanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa  Kabichi  Mhulu na waliweza kufanikiwa   kumkamata  akiwa  na fuvu la kichwa cha binadamu  akiwa amekihifadhi  ndani ya choo  alichokuwa akikitumia
 Alisema fuvu hilo alilokamatwa nalo alikuwa akilitumia   kwa ajiri ya  wateja wake  waliokuwa wakifika hapo  kwa ajiri ya matibabu  ambapo  walikuwa wakilikalia fuvu hilo wakati walipokuwa wakipatiwa matibabu yao
Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na polisi  kwa mahojiano zaidi  na anatarajiwa kufikishwa mahakamani  mara baada ya upelelezi  kukamilika  ili  kujibu tuhuma  inayomkabili

     
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa