Home » » HATARI: MWANAMKE AKAMATWA NA SARE ZA JESHI LA (JWTZ) NA ASKARI WA TANAPA

HATARI: MWANAMKE AKAMATWA NA SARE ZA JESHI LA (JWTZ) NA ASKARI WA TANAPA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mwanamke mmoja  Mkazi wa  Kijiji cha Ugala  Tarafa ya Ndurumo  Wilaya ya Mlele Mkoaa wa Katavi amekamatwa kwa tuhuma za kukamatwa akiwa na sare  ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  na sare  ya askari  za wanyama pori wa TANAPA
Mtuhumiwa huyo mwanamke  aliyekamatwa  alijulikana kwa jina la Ester John(21) Mkazi wa Kijiji hicho cha Ugala Wilaya ya Mlele
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari hapo jana kuwa mtuhumiwa  Ester  alikamatwa jana  majira ya  saa kumi jioni wakati akiwa nyumbani kwake
Kidavashari alisema muhumiwa huyo alikamatwa kufuatia taarifa za kutoka kwa raia wema ambao walitowa taarifa kwa jeshi la Polisi kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akihifadhi nguo hizo sare za jeshi na zimekuwa zikitumiwa na watu kwa ajiri ya kufanya uharifu
 Alisema baada ya taarifa hizo Polisi kwa kushirikiana na Askari wa TANAPA walikwenda Kwenye  Kijiji hicho cha Ugala kwa lengo la kufutilia  taarifa  hizo
Kidavashari alieleza baada ya kufika kijijini hapo  Askari hao walikwenda nyumbani kwa Mtuhumiwa  Ester kwa lengo la kumpekua nyumba yake hiyo
 Alisema  katika upekuzi walioufanya kwenye nyumba ya Mtuhumiwa Ester  waliweza kumkamata akiwa na  saruali  moja  na shati  moja la jeshi la wananchi  wa  Tanzania(JWTZ) pamoja  sare  pea moja  za askari  wa wanyama  pori TANAPA  na vyuma  viwili vya kutengenezea  risasi
Mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa tukio hilo utakapo kuwa umekamilika
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa