Home » » WANAWAKE WATAKIWA KWENDA HOSPITALI MAPEMA WAONAPO DALILI ZA SHINGO YA UZAZI

WANAWAKE WATAKIWA KWENDA HOSPITALI MAPEMA WAONAPO DALILI ZA SHINGO YA UZAZI


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka wanawake wote  hapa Nchini  waonapokuwa na dalili za kuwa na ungonjwa wa tezi ya shingo ya uzazi  salatani na festula   wawahi  mapema hospitali  ili  kuepukana na vifo vinavyotokana na  magonjwa hapo
Pinda alitowa wito huo hapo juzi wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji wa Mpanda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kashaulili Mjini  hapa
Alisema wanawake wengi  wamepoteza maisha  kutokana  na  chulewa  kufika  hospitali    kutibiwa ugonjwa wa tezi ya shingo na festula  na  salatani wakati wangewahi  kwenda hospitali  magonjwa hayo yanatibika
 Alifafanua   baadhi ya wanawake wamekuwa  wakiona aibu  kwenda  hospitali na kumwona    Daktari  na kumweleza    anaumwa nini  ili aweze  kupatiwa msaada wa matibabu
Wapo  wengine wanaogopa na kuona aibu kushikwa matiti na Daktari  wakati wanapimwa kansa ya ziwa  ugonjwa huo huwa haugunduluki  bila daktari kugusa  chuchu za maziwa alisema Pinda
 Alisema  yeye mwenyewe amekuwa  akiwapeleka   akina mama wengi ambao  wamekuwa na matatizo hayo lakini  kila anapowafikisha hospitali  wamekuwa wakiambiwa kuwa wamechelewa kufika hospitali na kupelekea kukatwa ziwa wakati wangewahi wangeweza kupona
Pinda  alisema  umefika wakati sasa wa akinamama  kubadilika  na  kuhakikisha  kila waonapo  dalili za kuwa na magonjwa hayo kuwahi  mapema pindi waonapokuwa  na dalili za ugonjwa
 Pia aliwataka  madaktari wote hapa  nchini kuwaelimisha wananchi na mapema madhara ya magonjwa hayo  kwani wapo baadhi ya akina mama  hawajuwi athari zake
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa