Home » » HOT NEWS: RAIA WAWILI WA NCHI YA BURUNDI WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO YA THAMANI MILIONI 148,500 ,000

HOT NEWS: RAIA WAWILI WA NCHI YA BURUNDI WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO YA THAMANI MILIONI 148,500 ,000


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
jeshi   la  Polisi Mkoani  Katavi linawashikilia watu wawili Raia wa Nchi ya Burundi kwa tuhuma za kuwakamata na meno ya tembo  vipande 25  vyenye uzito wa kilogramu  42 ikiwa ni sawa na tembo  sita yenye thamani ya shilingi milioni  148,500,000 wakiwa wamepatia kwenye basi la kampuni ya  AM l linalofanya safari zake kutoka Mpanda kwenda Mkoani Mwanza
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  amewataja watuhumiwa hao raia wa Nchi ya Burundi kuwa ni  Ndaisaba  Masoud(35) mkazi wa Kijiji cha  Katumba  makazi ya wakimbi ya Katumba Wilaya  ya Mlele  na  Samson Fred (25) mkazi wa Kijiji cha  Ivungwe Makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
 Watuhumiwa hao wote wawili walikamatwa hapo jana majira ya saa mbili na  robo  asubuhi  huko katika eneo la kijiji cha  Uruila  wakiwa wamepanda  basi la  kampuni ya A,M   lenye namba za usajiri  T,740 AQD lililokuwa likitoka Mpanda kuelekea  Mkoani  Mwanza
Kamanda Kidavashari alisema watuhumiwa hao wawili walikamatwa baada ya kutiliwa  mashaka na askari polisi wawili waliokuwa ndani ya basi hilo walilokuwa wakilisindikiza kutoka Mpanda  mjini
 Alisema  Polisi waliwatilia  shaka watuhumiwa hao baada ya kuwaona  wanaingiza ndani ya basi hilo  mabeji matatu makubwa  ndani ya basi hilo  huko katika eneo la Kijiji cha Uruila
Kidavashari alieleza  baada ya kuwatilia shaka watuhumiwa hao  polisi  walisimamisha safari ya basi hilo na ndipo walipoamua kufanya upekuzi  ndipo  walipo kuta mizigo hiyo ya watuhumiwa  wakiwa na nyara hizo za Serikali
 Alisema  watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na meno hayo ya  tembo walirudishwa hadi kwenye kituo cha polisi cha Wilaya ya Mpanda ambako bado wanaenelea  kushikiwa na Polisi kwa mahojiano zaidi
 Kamanda Kidavashari alisema  watuhumiwa hao wote wawili Raia wa Burundi wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika ili  waweze kujibu shitaka la kupatikana na nyara za Serikali
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa