Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imepanga kununua mitambo ya kutengenezea barabara yenye thamani ya Dola za Kimarekani 676,240
sawa na fedha za kitanzania kiasi cha
shilingi bilioni 1,149,608,000
Uamuzi wa kununua
mitambo hiyo ya kutengenezea barabara ulipishwa hapo jana kwenye baraza maaalumu la madiwani la
Halmashauri hiyo lililofanyika jana kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda uliopo mjini
hapa
Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo Estomikh Chang’ah alilieleza
baraza hilo la madiwani kuwa
fedha za kununulia mitambo hiyo
zimepatikana kufutia Halmashauri
ya Wilaya ya Mpanda kuPATIWA mkopo wa
fedha kutoka Benki ya TIB za kununulia
mitambo hiyo
Alisema katika ununuzi huo wa mitambo hiyo Halmashauri inatakiwa kulipa kwanza ndani ya siku
21 wawe wamelipa
kiasi cha Tsh 230,000,000 kwenye Benki ya TIB mkopo
huo ni wakipindi cha cha miaka mitano
Chan’gah aliitaja
mitambi hiyo itakayo nunuliwa kuwa ni
Greda Made 149K litakalogharimu kiasi cha dola za Marekani 436,600 sawa na Tsh milioni 742,200,000 na kijiko Model 320DL kwa gharama
ya dola 233,640 sawa na fedha Tsh milioni 397,188,000 na gharama za
kusafirishia mitambo hiyo itagharimu
kiasi cha shilingi milioni 10,200,000
Alilieleza Baraza hilo la madiwani kuwa hiyo itakuwa ni awamu ya kwanza ya
ununuzi wa mitambo hiyo ya kutengenezea barabara awamu ya pili itahusu ununuzi wa Shindilia
model cs 533e Boza la maji
na maloli mawili aina ya Tata
Diwani wa Kata
ya Kabungu Selemani Kasonso akichangia hoja kwenye baraza hilo alisema mradi huo wa mitambo ya kutengenezea barabara utaisadia sana halmashauri hiyo kujipatia kipato na kutengenezea barabara
zake nyingi za vijijini ambazo ni mbavu
Alisema
mradi huo endapo hauta
simamiwa vizuri unaweza kuwa
hauna manufaa yoyote kwenye halmashauri na matokeo yake
unaweza kuisababishia hasara Halmashauri
hiyo
Nae
Diwani wa viti maalumu Tiodela Kisesa
alieleza kuwa mitambo hiyo
itakapo nunuliwa ni vizuri
ikatumiwa kwa ajiri ya Halmashauri na
sio kwa ajiri ya kuwanufaisha watu
wachache kwa manufaa yao binafsi
Diwani wa Kata ya
Mpanda ndogo Hamad Mapengo aliliomba
Baraza hilo kuwahakikisha mchako huo wa ununuzi wa mitambo uwe ni wawazi kwa
kile alichohofia kuwa kunaweza kukawa na
udanganyika katika ununuzi badala ya kununua mitambo mipya ikanunuliwa mitambo
ya zamani
Kwaupande wake
Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Moshi
Kakoso alilieleza baraza hilo kuwa
mradi huo wa mitambo ya
kutengenezea barabara madiwani wasiuone kuwa ni mdogo
Alisema
Halmashauri nyingi hapa nchini
hazina mitambo kama hiyo hivyo Halmashauri kununua mitambo hiyo itakuwa
imewajengea heshima kubwa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment