Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mwenyekiti wa
kitongoji cha Mwangaza (CCM) Kijiji cha Ipwaga Kata
ya Ilele Tarafa ya Inyinga Wilaya ya Mlelele Mkoani hapa Makomba
Budimba (39)ambae alichaguliwa
hivi karibuni katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika
Desemba 14 mwaka jana na kuchaguliwa kukiongoza kitongoji hicho ameuwawa kikatili kwa kupigwa risasi kifuaani na shingoni na watu wwawili wasio
fahamika nyumbani kwake
Kwa mujibu wa ofisa
mtendaji wa kata hiyo ya Ilele Jackisin Fyula
tukio la mauwaji ya kikatili ya mwenyekiti huyo lilitokea hapo Jana majira ya saa nane usiku akiwa nyumbani
kwake
Siku hiyo ya
tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mke wake ndipo ilipofikia majira ya saa nane usiku walifika nyumbani kwa marehemu watu wawili wasiofahamika wakiwa na pikipiki aina
ya Sunlg namba ambazo zikuweza kufahamika
Fyula
alisema baada ya watu hao wawili kufika
nyumbani kwa marehemu walimuomba marehemu
afungue mlango wa nyumba yake kwa kile walidai kuwa wanashida na
yeye ya muhimu usiku huo
Baada ya watu hao
kuomba marehemu awafungue mlango mkewe
alimsihi marehemu asifungue mlango
kwani wanaweza kuwa watu na nia mbaya ya kumzuru
Alisema
marehemu mbali ya kushauri na
mkewe aliona ni busara
kufungua mlango na kutoka nje kuwasikiliza shida yao watu hao ambao alidhani walikuwa wakihitaji huduma
yake kama kiongozi wa kitongoji hicho
Alileza
ndipo marehemu alipofungua mlango wa nyumba na kisha akiwa amesimama katikati ya mlango wa nyumba
yake alishambuliwa kwa kupigwa risasi
kifuani na shingoni kwa bunduki aina ya SMG na kufariki Dunia hapo hapo
Alisema baada
ya kufanya mauwaji hayo ya kikatili watu hao walitokomea
na pikipiki yao mahari kusiko julikana
hata hivyo taarifa za mauwaji hayo ziliwafikia majirani na wananchi wa
kijiji hicho ambao waliweka vizuizi za
kuweka magongo kwenye barabara zote za kitongoji hicho zinazoingia na kutoka
Alieleza hata
hivyo watu hao walifanikiwa kuvuka kwenye
vizuizi vilivyokuwa viwekwa kwenye njia
hizo kwa kutumia pikipikiyao hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela amekili kupoke
taarifa ya mauwaji ya mwenyekiti huyo
wa kitongoji cha Mwangaza Kata ya Mlele
Alisema mpaka sasa hakuna watu waliokamatwa
kuhusiana na mauwaji hayo na juhudii za kuwasaka waliohusika na mawaji
zinaendelea kwa jeshi la polisi kwa
kushirikiana na wananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment