Tuesday, January 13, 2015

MWENYEKITI WA KITONGOJI(CCCM)AUWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA SHINGONI‏

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mwenyekiti wa kitongoji cha  Mwangaza (CCM)  Kijiji cha Ipwaga     Kata ya Ilele Tarafa ya Inyinga Wilaya ya Mlelele Mkoani hapa  Makomba  Budimba  (39)ambae  alichaguliwa  hivi  karibuni katika  uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14 mwaka jana na kuchaguliwa kukiongoza kitongoji hicho ameuwawa  kikatili  kwa kupigwa risasi  kifuaani na shingoni na watu wwawili wasio fahamika   nyumbani kwake
Kwa mujibu wa ofisa mtendaji wa kata hiyo ya Ilele Jackisin Fyula  tukio la mauwaji ya kikatili ya mwenyekiti huyo  lilitokea hapo  Jana majira ya saa nane usiku akiwa nyumbani kwake
Siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mke wake ndipo ilipofikia  majira ya saa nane usiku  walifika nyumbani kwa marehemu  watu  wawili wasiofahamika wakiwa na pikipiki aina ya Sunlg namba ambazo zikuweza kufahamika
Fyula alisema  baada ya watu hao wawili kufika nyumbani kwa marehemu  walimuomba  marehemu  afungue mlango wa nyumba yake kwa kile walidai kuwa wanashida na yeye  ya muhimu usiku huo
Baada ya watu hao kuomba marehemu awafungue mlango  mkewe alimsihi  marehemu asifungue mlango kwani  wanaweza kuwa watu  na nia mbaya ya kumzuru
 Alisema  marehemu mbali ya kushauri  na mkewe  aliona ni  busara  kufungua mlango na kutoka nje kuwasikiliza shida yao watu hao  ambao alidhani walikuwa wakihitaji huduma yake kama kiongozi wa kitongoji  hicho
 Alileza  ndipo marehemu alipofungua mlango wa nyumba   na kisha akiwa  amesimama katikati ya mlango wa nyumba yake  alishambuliwa kwa kupigwa risasi kifuani na shingoni kwa bunduki aina ya SMG na kufariki Dunia hapo hapo
Alisema baada ya  kufanya  mauwaji hayo ya kikatili watu hao walitokomea na pikipiki yao mahari kusiko julikana  hata hivyo taarifa za mauwaji hayo ziliwafikia majirani na wananchi wa kijiji  hicho ambao waliweka vizuizi za kuweka magongo kwenye barabara zote za kitongoji hicho zinazoingia na kutoka
Alieleza hata hivyo watu hao walifanikiwa  kuvuka kwenye vizuizi vilivyokuwa viwekwa kwenye  njia hizo kwa kutumia pikipikiyao hiyo
Mkuu wa  Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela amekili kupoke taarifa ya   mauwaji ya mwenyekiti huyo wa kitongoji cha Mwangaza Kata ya Mlele
 Alisema mpaka sasa hakuna watu waliokamatwa kuhusiana na mauwaji hayo na juhudii za kuwasaka waliohusika na mawaji zinaendelea kwa  jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment