Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu blog
jeshi la
Polisi Mkoani Katavi
linawashikilia watu wawili Raia wa Nchi ya Burundi kwa tuhuma za kuwakamata na
meno ya tembo vipande 25 vyenye uzito wa kilogramu 42 ikiwa ni sawa na tembo sita yenye thamani ya shilingi milioni 148,500,000 wakiwa wamepatia kwenye basi la
kampuni ya AM l linalofanya safari zake
kutoka Mpanda kwenda Mkoani Mwanza
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amewataja watuhumiwa hao raia wa Nchi ya
Burundi kuwa ni Ndaisaba Masoud(35) mkazi wa Kijiji cha Katumba
makazi ya wakimbi ya Katumba Wilaya ya Mlele na
Samson Fred (25) mkazi wa Kijiji cha
Ivungwe Makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Watuhumiwa hao wote wawili walikamatwa hapo
jana majira ya saa mbili na robo asubuhi
huko katika eneo la kijiji cha
Uruila wakiwa wamepanda basi la
kampuni ya A,M lenye namba za
usajiri T,740 AQD lililokuwa likitoka
Mpanda kuelekea Mkoani Mwanza
Kamanda
Kidavashari alisema watuhumiwa hao wawili walikamatwa baada ya kutiliwa mashaka na askari polisi wawili waliokuwa
ndani ya basi hilo walilokuwa wakilisindikiza kutoka Mpanda mjini
Alisema
Polisi waliwatilia shaka watuhumiwa
hao baada ya kuwaona wanaingiza ndani ya
basi hilo mabeji matatu makubwa ndani ya basi hilo huko katika eneo la Kijiji cha Uruila
Kidavashari
alieleza baada ya kuwatilia shaka
watuhumiwa hao polisi walisimamisha safari ya basi hilo na ndipo
walipoamua kufanya upekuzi ndipo walipo kuta mizigo hiyo ya watuhumiwa wakiwa na nyara hizo za Serikali
Alisema
watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na meno hayo ya tembo walirudishwa hadi kwenye kituo cha
polisi cha Wilaya ya Mpanda ambako bado wanaenelea kushikiwa na Polisi kwa mahojiano zaidi
Kamanda Kidavashari alisema watuhumiwa hao wote wawili Raia wa Burundi
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika
ili waweze kujibu shitaka la kupatikana
na nyara za Serikali
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment