Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Watu wasiofahamika wamefukua kabuli na
kubeba mwili wa marehemu aliyekuwa
amezikwa kwenye makaburi ya Isanjsndugu
Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele
Mkoani Katavi kwa kile kinachodaiwa
kuwa ni imani za kishirikina
Kwa mujibu wa
Diwani wa Kata ya Nsimbo Michael Kasanga(CCM) alisema tukio hilo la imani za
kishilikina lilitokea hapo juzi kwenye makaburi ya Isanjandugu
Tarafa ya Nsimbo
Alisema kabuli la marehemu huyo ambalo lilifukuliwa
na watu wasiojulikana ililigunduliwa hapo juzi na wananchi wawili
waliokuwa wanakwenda
shambani ambao walipita jirani na
makabuli hayo na kuona kabuli hilo limefukuliwa
Diwani Kasanga alieleza baada ya wananchi hao wawili kuona kabuli
hilo limefukuliwa walishitushwa
na hari hiyo na iliwalazimu kurudi
kijijini na kutoa taarifa kwa uongozi wa
serikali ya kijiji
Alisema baada ya viongozi wa Kijiji hicho kupata taarifa hiyo
waliongozana na baadhi ya wananchi kwenda kwenye maeneo hayo ya mababuri ya
Kijiji hicho
Baada ya kufika kwenye eneo hilo la kabuli
hilo walikuta limefukuliwa na watu ambao hawejafamika huku
mabaki ya mwili wa marehemu huyo
yakiwa yamebebwa kwa kile
kinachoonekana ni imani za kishirikina
Alisema
kabuli hilo lilishindwa kufahamika jina la marehemu aliyekuwa amezikwa kwenye kabuli hilo
kutonana na kile kilichoonekana kuwa
kabuli hilo lilikuwa ni la muda mrefu
Diwani Kasanga alifafanua kuwa imekuwa ni
tabia ya muda mrefu kwa wananchi wa
Kijiji hicho kuwa na tabia ya
kwenda kwenye makabuli hayo mida ya usiku na kuoga dawa za kienyeji juu
ya makabuli kwa imani za kishilikina
Alisema
anatowa wito kwa wananchi wa Kijiji hicho kuacha tabia hiyo ya kuchezea
kwenye makabuli na kuogea dawa kwani tabia
hiyo ya imani potofu sio
nzuri kwenye jamii
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment