Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Katika hari
ambayo haikutarajiwa mtafahaluku
mkubwa umetokea hapo jana katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi baada ya ndugu wanne wa familia moja
wakiongozwa na mama yao mzazi kufanya
vurugu katika mahakama hiyo wakitaka
kumchomoa ndugu yao mikononi mwa Polisi aitwaye Maiko Edward(22)ili asiende kutumikia
kifungo cha maisha jela baada ya kuhukumiwa
na mahakama hiyo hiyo kifungo cha maisha
jela kwa kosa la kulawiti mtoto
wa kiume(79)
Ndugu hao wafanya
mtafaharuku huo wametajwa kuwa ni Deo Edward(25) Ferista Edward(23), Nicodemas Edward(19) pamoja na
mama yao mzazi aitwaye Fortunata
Kasosa(40)wote wa kazi wa mjiwa Mpanda
Mtaruku huo ulitokea mara baada ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa kutowa hukumu ya ndugu
yao ambae alihukumiwa kifungo cha maisha jela baadaya kupatikana na kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka
saba mkazi wa mtaa wa Nsemlwa Mjini hapa
Baada ya kutolewa
kwa hukumu hiyo polisi walimchukua kutoka kizimbani mshitakiwa Maiko Edward kwa
lengo la kumpatia kwenye gari lao
iliwaweze kumpeleka magereza
kwenda kutumikia kifungo chake hicho cha maisha
Wakati polisi wakiwa wanatoka nae nje ya jengo
la mahakama ndugu hao waliwazuia Polisi kwenda nae kwenye gari huku wakitowa
maneno kuwa endi mtu kufungwa magereza
hari ambayo ilisababisha mtafaruku mkubwa baina ya ndugu hao na askari polisi.
Kutokana na hari
hiyo polisi walifanikiwa kutuliza hari hiyo na waliweza kuwaweka chini ya
ulinzi wanafamilia hao na kisha walipelekwa kituo cha polisi cha Wilaya ya
Mpanda
Wanafamiliahao
kisha walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kufanya vurugu
mahakamani na kuwazuia polisi kufanya kazi na mwandesha mashitaka Kurwa
Sikwesa mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa.
Washitakiwa hao
wanne walikana mashitaka hayo na walikwenda rumande hadi hapo Januari 29 baada ya kushindwa kutimiza
mashariri ya mdhamana
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment