Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mpiga
debe kwenye stendi ya mabasi ya
mji wa Mpanda Mkazi wa Mtaa wa Mji wa
Zamani Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi Maiko
Edward (BAROTI) 25 amehukumiwa
kifungo cha maisha jela
baada ya kupatikana na hatia ya
kumbaka mtoto wa kiume mwenye umri wa
miaka saba mkazi wa mtaa wa Nsemlwa
ambae jina lake tunalo
Hukumu hiyo iliyovutia hisia za watu wengi wa mji wa Mpanda ilitolewa juzi na Hakimu mkazi Mfawidhi
wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda
Chiganga Ntengwa baada ya
mahakama kulidhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo wa pande
mbili za mashitaka na utetezi
Awali
akisoma maelezo ya upande wa
mashitaka mwendesha mashitaka Kurwa
Sikwesa alidai Mahakamani hapo
kuwa mshitakiwa Maiko Edward alitenda kosa hilo hapo Oktoba
9 ,2014 majira ya saa kumi na mbili jioni katika eneo la mji wa zamani
Alisema siku hiyo ya tukio mshitakiwa
alikutana na mtoto huyo njiani
wakati alikuwa akielekea nyumbani
kwa wazazi wake huko katika mtaa wa
Nsemlwa ndipo alipomshika mkono mtoto
huyo na kisha kwenda nae kwenye pagala
la nyumba lililokuwa katika mtaa
wa Mji wa Zamani
Mwendesha mashitaka alidai kuwa baada ya
kufika kwenye pagala hilo la nyumba
mshitakiwa alishikisha mkononi
mtoto huyo kipande cha mbao na kisha aliingia ndani ya chumba kimoja kilichokuwa
kwenye pagala hilo
Alieleza
baada ya kuingia nae ndani ya chumba hicho mtuhumiwa alitowa kisu na kuchoma kwenye ubao aliokuwa ameshika
mtoto huyo ikiwa ni ishara ya kumtishia kisha alimwambia endapo atakata kulawitiwa au
akipiga kelele atamuuwa kwa kumchoma na kisu kama alivyofanya kuchoma kisu ubao huo
Mwendesha
mashitaka alidai kuwa ndipo mtuhumiwa Maiko
Edwadr alipomvua mtoto huyo kaputula yake na kisha
yeye alivua saruali yake na
kutowa uume wake na kuupaka mate na kisha kuanza kumlawiti mtoto huyo kwa
nguvu mpaka alipomaliza haja yake
Alidai mahakamani hapo kuwa baada ya kumlawiti mtoto huyo alimtishia
tena kuwa endapo atamwambia mtu yoyote
kitendo hicho alichomfanyia atamuuwa
hata hivyo mtoto huyo baada ya kufika kwa wazazi wake alilazimika kuwaambia kutokana na hari ya maumivu aliyokunayo
Wazazi wake walimuuliza kama anaweza kuwa anamfahamu mtu
aliyemfanyia kitendo hicho ndipo alimtaja kuwa ni mtuhumiwa Maiko Edward ndipo wazazi wake
na mtoto walipokwenda kituo cha
polisi cha Wilaya ya Mpanda na kutoa
taarifa kisha walimpeleka katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambapo kutokana na hari mbaya aliyokuwa nayo
mtoto huyo alilazimika kulazwa
Alisema
jitihada za kumtafuta mshitakiwa zilianza ambapo siku moja mtoto huyo alipokuwa amekaa nyumbani kwao akiwa na mama yake alimwona mshitakiwa Maiko akipita karibu na
nyumba yao na ndipo alipokimbia na kujifisha nyuma ya mgongo wa mama yake ambae
alimuuliza anajificha nini na ndipo alipomjibu kuwa anamwogopo mshitakiwa kwani alimwammbia wakati anamlawiti
kuwa atamuuwa
Alieleza
ndipo mamayake alipokwenda kituo
cha polisi kutoa taarifa ya kuwa yule mtuhumiwa aliyekuwa anatafutwa ameonekana
ndipo polisi walipofanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa kwenye eneo la stendi ya mabasi aliko kuwa akifanyia kazi ya kupiga
debe
Mshitakiwa katika utetezi wake mshitakiwa
aliomba mahakama imwachie huru
kwani yeye hakutenda kitendo
hicho na wala alikuwa hamfahamu kabisa
mtoto huyo aliyelawitiwa
Baada ya utetezi huo Hakimu Chiganga
Ntengwa allisoma hukumu hiyo kwa kueleza kuwa mahakama bila kuwa na shaka yoyote imemuona mshitakiwa
Maiko Edward kuwa amepatikana na hatia ya kulawiti mtoto kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani
hapo wa mtoto mwenyewe pamoja na Daktari
Hivyo mshitakiwa
amepatikana na kosa la kifungu cha
sheria namba(154) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2009 kutona na kosa
hilo adhabu yake inatokana na
kifungu cha sheria namba
235 sura ya 20 ya marekebisho ya
mwaka 2009 kwa kwahiyo mahakama kuanzia
jana imemuhukumu Maiko Edward kwenda jela kifungo cha maisha
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment