Sunday, January 18, 2015

MADIWANI WATAKIWA KUPIMA MAAMBUKIZI YA VVU‏


Na  Walter Mguluchuma
Katavi
Madiwani  wa  Halmashauri ya Nsimbo  katika Wilaya ya Mlele  Mkoa wa   Katavi  ambao wanamaliza muda wao mwaka huu wameshauri kupimwa kwanza maambukizi ya VVU  kabla ya kuchukua fomu za kugombea Udiwani kwenye Kata zao  ili waweze  kutambua afya zao  na kujua kama watakuwa na nguvu za kutosha kuwatumikia wananchi wao  kwa kipindi kijacho
Ushauri huo ulitolewa juzi na Diwani  wa Kata ya Kapalala  Reward Sichone   kwenye kikao cha Baraza la Madiwani  la Halmashauri ya Nsimbo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo
 Sichone alisema ni  vizuri kwa madiwani wa Halmashauri hiyo wanao maliza muda wao mwaka huu wakaandaliwa utaratibu na Halmashauri hiyo wa kupimwa maambukizi ya VVU kabla ya kumaliza muda wao wa uongozi mwaka huu
 Alilieleza Baraza hilo la  madiwani kuwa  endapo  watapimwa afya zao  mapema  itawafanya wajitathimini  kabla ya kuchukua fomu za kugombea  udiwani kwenye Kata zao za sasa
 Sichone alisema  endapo diwani atapimwa na kukutwa anamatatizo kwenye  afya yake  itamsadia  kuona kama kweli atakuwa na uwezo wa nguvu za kufanya kazi za wananchi  kwenye eneo  lake
 Aliwafafanulia kuwa haitakuwa vizuri kwa diwani ambae atakae pimwa na kukutwa  na maambukizi ya VVU  halafu  achukue fomu za kugombea tena wakati anajua kuwa  ana matatizo ya afya yake  hari  ambayo   itamfanya  kutokuwa na  nguvu za kufanya kazi za wananchi wake   hivyo swala la madiwani kupima  afya zao ni jambo la msingi sana
 Kwa upande  mwenyekiti  wa kamati ya kudhibiti  ukimwi  wa  Baraza hilo la Madiwani  Sylvester Nswima  ambae pia ni Diwani wa Kata ya Sitalike alipinga  ushauri huo wa Diwani Sichone
Nswima alilieleza swala hilo la madiwani wa Halmashauri hiyo kupimwa afya zao haiwezekani kwani kupima ni  hiyari ya kila mtu na sio lazima
Nae Mwenyekti wa  Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Assenga alieleza kuwa  kitendo cha wao madiwani kupima afya zao  kinaweza kuwa  ni mfano mzuri kwa watumishi  wa Halmashauri  hiyo na wananchi wa Halmashauri hiyo kuwaona viongozi wao wakimwa afya zao  na kuwafanya nao waige
 Alisema  madiwani tusihofu kupimwa   bali tuangalie utaratibu wa  kuwaita wataalamu waje watupime afya  ili tuwe mfano kwa watu wengine  kwenye Halmashauri hiyo  na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wake  alieleza Assenga
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment