Sunday, January 18, 2015

HALMASHAURI YA NSIMBO IMEPANGA KUPUNGUZA VIFO VYA WAZAZI


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoani  Katavi  imepanga kupunguza vifo vya  Wazazi  kutoka  vifo  83 kwa  100,000 vya  mwaka  2012 na 2013 hadi kufikia  vifo  75 kwa 100,000 ifikapon june  2015
Hayalisemwa  na mwenyekiti wa  kamati ya  elimu  Afya na  Maji  wa Baeaza la madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo  Raphael Kalinga  wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo  kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika juzi kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Nsimbo
Diwani Kalinga  alisema  Halmashauri hiyo imeweka malengo ya kuhakikisha inapunguza vifo vya wazazi na watoto wadogo chini ya mwezi mmoja na chini ya miaka mitano
Alieleza  Halmashauri imepanga kupunguza  vifo vya watoto  wachanga  wa siku 0  hadi siku 28 kutoka vifo vya watoto  6 kwa 1000 vya mwaka  2012 na 2013 hadi kufikia vifo viwili  kwa elfu moja ifikapo  june 2015
Vifo vya watoto  chini ya  miaka mitano  kutoka vifo kumi na sita kwa  elfu moja vya mwaka 2012 na 2013 na  kufikia vifo  kumi na mbili ifikapo june 2015
 Alieleza lengo la Halmashauri hiyi  pia ni kuongeza  idadi ya akinamama  wajawazito wanaojifungulia  katika vituo vya   kutolea huduma  za Afya  toka asilimia hamsini  na sita  ya mwaka 2012 na 2013 na kufikia  asilimia 65 june mwaka huu ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo vya kutplea huduma ya afya ili kuweza kuokoa uhai wa mama na mtoto
Pia kuongeza  kiwango  cha kutumia  huduma  za kisasa  za uzazi  wa mpango  kutoka asilimia  34 ya mwaka 2012 na 2013 na kufikia asilimia  sitini na tano  hadi ifikapo june mwaka  huu
Kalinga  alieleza  lengo jingine ni kuongeza  kiwango cha  kutumia  chanjo  chanjo zte   kinafikia  wastani  wa asilimia  tisini na tano na zaidi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment