Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya
Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoani
Katavi imepanga kupunguza vifo
vya Wazazi kutoka
vifo 83 kwa 100,000 vya
mwaka 2012 na 2013 hadi kufikia vifo 75 kwa 100,000 ifikapon june 2015
Hayalisemwa na mwenyekiti wa kamati ya
elimu Afya na Maji
wa Baeaza la madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo Raphael Kalinga wakati alipokuwa akiwasilisha taarifa ya
kamati hiyo kwenye kikao cha Baraza la
madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika juzi kwenye ukumbi wa Halmashauri
ya Nsimbo
Diwani
Kalinga alisema Halmashauri hiyo imeweka malengo ya
kuhakikisha inapunguza vifo vya wazazi na watoto wadogo chini ya mwezi mmoja na
chini ya miaka mitano
Alieleza Halmashauri imepanga kupunguza vifo vya watoto wachanga
wa siku 0 hadi siku 28 kutoka
vifo vya watoto 6 kwa 1000 vya
mwaka 2012 na 2013 hadi kufikia vifo
viwili kwa elfu moja ifikapo june 2015
Vifo vya
watoto chini ya miaka mitano kutoka vifo kumi na sita kwa elfu moja vya mwaka 2012 na 2013 na kufikia vifo
kumi na mbili ifikapo june 2015
Alieleza lengo la Halmashauri hiyi pia ni kuongeza idadi ya akinamama wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya
toka asilimia hamsini na
sita ya mwaka 2012 na 2013 na
kufikia asilimia 65 june mwaka huu ya
akina mama wanaojifungulia kwenye vituo vya kutplea huduma ya afya ili kuweza
kuokoa uhai wa mama na mtoto
Pia kuongeza kiwango
cha kutumia huduma za kisasa za uzazi
wa mpango kutoka asilimia 34 ya mwaka 2012 na 2013 na kufikia
asilimia sitini na tano hadi ifikapo june mwaka huu
Kalinga alieleza
lengo jingine ni kuongeza kiwango
cha kutumia chanjo
chanjo zte kinafikia wastani
wa asilimia tisini na tano na
zaidi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment