Home » » WATUMISHI WA MIFUGO WAAGIZWA KWENDA VIJIJINI KUWAELISHA WAFUGAJI

WATUMISHI WA MIFUGO WAAGIZWA KWENDA VIJIJINI KUWAELISHA WAFUGAJI


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amewaagiza watumishi wa Idara ya Mifugo na Uvuvi  wa  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kuacha mara moja tabia ya kushinda ofisini na badala yake waende vijijini wakawafundishe wafugaji  nanma ya ufugaji bora wa mifugoili  wafugaji waipende Serikali
 Agizo hilo  alilitowa hapo jana wakati alipotembelea kukagua mradi wa  mtambo  wa kuzalisha   kimiminika  cha Naitrojeni  kitakachotumika  katika  kuhifadhi  mbegu  bora za mifugo  katika eneo la  jengo la ofisi ya Idara hiyo Mjini hapa
 Alisema wataalamu wa kilimo waache tabia ya kushinda ofisini na badala yake waende vijijini wakatoe elimu kwa wafugaji itakayo wasaidia  wafugaji  kuwa na  ufugaji bora wa kisasa na wenye tija
 Alisema endapo wafugaji wataelimishwa na wataalamu wa mifugo namna ya ufugaji bora na wakisasa itawafanya wafugaji  waelewe maana ya ufugaji bora na kuwafanya wafugaji waipende Serikali  badala ya kuichukia
Mwamlima alisema kumekuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara wa  baina ya Serikali na wafugaji  hasa pale wafugaji wa mifugo wanapokuwa wamevamia maeneo ya hifadhi ya mistu na vyanzo vya maji
 Alifafanua endapo wafugaji wataelimishwa  nanma ya  ufugaji  bora na wakisasa na matumizi bora ya ardhi tatizo la migogoro ya wafugaji na Serikali halitakuwepo tena kwani wafugaji watakuwa wameisha elimlika  na wataendelea kuipenda Serikali
Alisema  wafugaji wanapokuwa wamevamia maeneo ya  hifadhi ya mistu na  Serikali  inapowataka wahame kwenye maeneo hayo  wamekuwa wakiona kama vile Serikali inawaonea  wakati  sio hivyo  na matokeo yake wamekuwa wakiiona Serikali kama ni adui yao
 Alieleza  waemisheni wafugaji ili waione Serikali kuwa ni rafiki yao  kuliko ilvyo sasa ambapo wakiwaona viongozi wa Serikali kwenye maeneo yao wamekuwa wakiwakimbia
 Aliwataka pia wataalamu hao wa mifugo na uvuvi  kuwaelimisha wafugaji  waanache na tabia ya kuhamaama kiolela
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa