Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Paza Mwamlima amewaagiza watumishi wa Idara ya Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kuacha mara
moja tabia ya kushinda ofisini na badala yake waende vijijini wakawafundishe
wafugaji nanma ya ufugaji bora wa mifugoili wafugaji waipende Serikali
Agizo hilo alilitowa hapo jana wakati alipotembelea
kukagua mradi wa mtambo wa kuzalisha
kimiminika cha Naitrojeni kitakachotumika katika
kuhifadhi mbegu bora za mifugo katika eneo la jengo la ofisi ya Idara hiyo Mjini hapa
Alisema wataalamu wa kilimo waache tabia ya
kushinda ofisini na badala yake waende vijijini wakatoe elimu kwa wafugaji
itakayo wasaidia wafugaji kuwa na ufugaji bora wa kisasa na wenye tija
Alisema endapo wafugaji wataelimishwa na
wataalamu wa mifugo namna ya ufugaji bora na wakisasa itawafanya wafugaji waelewe maana ya ufugaji bora na kuwafanya
wafugaji waipende Serikali badala ya
kuichukia
Mwamlima alisema
kumekuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara wa
baina ya Serikali na wafugaji hasa pale wafugaji wa mifugo wanapokuwa
wamevamia maeneo ya hifadhi ya mistu na vyanzo vya maji
Alifafanua endapo wafugaji wataelimishwa nanma ya
ufugaji bora na wakisasa na
matumizi bora ya ardhi tatizo la migogoro ya wafugaji na Serikali halitakuwepo
tena kwani wafugaji watakuwa wameisha elimlika
na wataendelea kuipenda Serikali
Alisema wafugaji wanapokuwa wamevamia maeneo ya hifadhi ya mistu na Serikali
inapowataka wahame kwenye maeneo hayo wamekuwa wakiona kama vile Serikali inawaonea wakati
sio hivyo na matokeo yake
wamekuwa wakiiona Serikali kama ni adui yao
Alieleza
waemisheni wafugaji ili waione Serikali kuwa ni rafiki yao kuliko ilvyo sasa ambapo wakiwaona viongozi
wa Serikali kwenye maeneo yao wamekuwa wakiwakimbia
Aliwataka pia wataalamu hao wa mifugo na
uvuvi kuwaelimisha wafugaji waanache na tabia ya kuhamaama kiolela
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment