Na Walter Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa ni Katavi kwa kushirikiana na
Wizara ya Mifugo na uvuvi
imeweza kupa ta na kufunga mtambo
wa kuzalisha kimiminika cha Naitrojeni itakayo tumika katika
kuifadhi mbegu bora za
mifugo kwa ajiriya uhamilishaji mifugo
wenye thamani ya shilingi milioni 400
Hayo yalielezwa hapo jana na Afisa Mifugo wa Idara ya Mifufo na uvuvi Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Laulenti
Elias mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima wakati alipo tembelea kukagua
mtambo huo wa kisasa uliopokwenye jengo la Idara ya Mifugo na uvuvi
Mjini hapa
Alisema
mtambo huo ililetwa Wilayani Mpanda
mwezi june 2014 na usimikaji wake
ulikamilika mwezi Septemba gharama yake umegalimu kiasi cha shilingi milioni 400 na garama ya
usimikaji wa mtambo huo umegharimu kiasi cha shilingi Tsh37,290,950 na kufanya gharamu kuwa ya
jumla ya shilingi milioni 437,290,000kwa
mradi huo hadi sasa
Alifafanua
kuwa mtambo huo wa Cryomech 120
unauwezo wa kuzalisha lita tano
za kimiminika cha Naitrojeni
kwa saa moja kiasi hicho
huzalishwa baada ya muda
wa kuwa tayari baada ya mtambo
kuwashwa
Alisema Wilaya ya Mpanda pamoja kuwa
na idadi kubwa ya mifugo iliyopo
bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazo ikabiri Idara ya Mifugo
na uvuvi Wilayani hapa ambazo alizitaja baadhi ya changamoto hizo
kuwa ni
Uzalishaji
mdogo wa mazao ya mifugo
kama vile nyama na maziwa
,upatikanaji mdogo wa mbegu bora
za mifugo hususani Ng’ombe
Changamoto nyingine ni kuwepo kwa eneo dogo la malisho
ukilinganisha na idadi ya mifugo iliyopo Wilayani hapa pamoja na
kuwepo kwa magojwa mengi ya mifugo mfano
ndorobo,ndigana kali na homa
ya mapafu
Nae Mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’ah alisema mtamba huo ni wanne kufungwa hapa nchini mitambo mingine kama
hiyo ipo katika mikoa ya Mbeya .Arusha na Iringa
Alisema
Halmashauri yake imeandaa utaratibu
utakao wawezesha wafugaji kupatiwa mafunzo yatakayo wasaidia kujifunza nanma ya kuzalisha
Kimiminika cha Niaitrojeni
Alieleza
pia watautumia mtambo huo kwa ajiri kama mradi kwa ajiri ya wafugaji wa kutoka
katika Mikoa ya jirani watakao kuwa wanakwenda kujifunza hapo
Kwa upande wake
mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima
aliwataka viongozi wa Halmashauri
kuufanya mradi huu kuwa ni mradi
endelevu
Alisema mradi huo
umegharimu fedha nyingi hivyo atashangaa kusikia baada ya muda fulani mradi huo
kuwa umesimama sitaki itokea kama
ilivyotokea kwa mradi wa mashine ya kukoboa mpunga wa Mwamapuli Tarafa ya Mpimbwe ulivyoshindwa kufanya kazi
kwa kipindi cha miaka sita sasa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment