Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mwanamke
mmoja aliyejulikana kwa jina la
Agnes Sikazwe (28) Mkazi wa
Kijiji cha Majimoto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amekatwa
masiko yake yote mawili kwa
kisu na mume wake aliyejulikana kwa jina la Ndomo Mwandu(32)
mkazi wa kijiji cha Maji moto baada ya
kumtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi
na mwanaume mwingine
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo la kukatwa masikio kwa mwanamke huyo lilitokea hapo Novemba 8
majira ya saa sita na nusu usiku nyumbani kwa wanandoa hao wawili waliokuwa
wakiishi pamoja
Alisema kabla ya tukio hilo wanandoa
hao wawili walikuwa na ugomvi wa mara
kwa mara wa muda wa mrefu
ambapo Ndomo Mwandu alikuwa akimtuhumu Agnes
Sikazwekuwa alikuwa na mahusiano
ya kimapenzi na mwanaume mwingine
kijijini hapo
Kidavashari
alieleza siku hiyo ya tukio wanandoa
hao wawili walikuwa
wamelala kitandani ndipo
mtuhumiwa Ndomo Mwandu alipoanza kumtuhumu Agnes
kuwa bado anaendelea na mahusiano
ya kimapenzi na mwanaume mwingine kijijini hapo
Alisema
wanandoa hao waliendelea kuzozana
kwa muda mrefu wakiwa kitandani hapo na kisha Agnes alipitiwa na usingizi na kisha alilala
usingizi
Alieleza
ndipo mtuhumiwa Ndomo alipoamka kitandani wakati huo Agnes akiwa anaendelea kupiga usingizi na alichukua
kisu na kisha kumkata
masikio yake yote mawili na kisha
kukimbia kusiko julikana
Baada ya kufanyiwa kitendo hicho
Agnes alipiga mayowe yakuomba
msaada kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo na kumkuta Agnes akiwa amekatwa masikio yake
yote mawili huku mtuhumiwa akiwa ameisha tokomea kusiko julikana
Majirani
walimchukua Agnes na kumpeleka kwenye kituo
cha Afya cha Usevya kwa ajiri ya kupatiwa matibabu ambapo amelazwa huku
hari yake ikiwa inaendelea vizuri
Kamanda Kidavashari alisema
uchuguzi uliofanywa na jeshi la polisi
umebaini kuwa chanzo cha tukio hili ni
wivu wa kimapenzi na
mtuhumiwa Ndomo Mwandu bado haja kamatwa kwani
baada ya kutenda tukio hilo
alikimbia kusiko julikana
Jeshi la Polisi linaendelea
na upelelezi ili kubaini alikokimbilia
mtuhumiwa ili waweze
kumkamata na kumfikisha Mahakamani ili aweze
kujibu tuhuma inayomkabili
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment