Tuesday, December 9, 2014

WAKINA MAMA WATATU WAFARIKI WAKIWA WANAJIFUNGUA HUKO INYONGA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Akinamama wajawazito watatu  wamefariki Dunia Wilayani Mlele Mkoani  Katavi  wakati wakujifungua katika kituo cha Afya cha Inyonga  na  Mamba  kutokana na sababu mbalimbali  ikiwepo  kutokkwa na damu nyingi wakati wa kujifungua katika kipindi cha mwezi  septemba 2014  hadi  hadi Novemba  mwaka huu   

 Mraribu  wa  Afya yaMama  na Mtoto   wa  Wilaya  ya  Mlele  Lucy  Songoro  alisema hayo hapo jana  alipokuwa  akitowa taarifa mbele ya mwandishi wa habari hizi kuhusiana na taarifa ya vifo vilivyo tokea  katika   kituo ch  Afya  cha Inyonga kwa kipindi miezi mitatu ya Septemba hadi Novemba
Alisema katika vifo hivyo  vitokanavyo na uzazi   wajawazito wawili  alifariki  mwezi  wa  Septemba  katika kituo cha  Afya cha Inyonga na  Mamba  kutokana na  kutokwa na  damu nyingi  kabla ya kujifungua 

 Alifafanua kuwa katika kipindi cha mwezi  uliofuata yaani mwezi Oktoba  alifariki mama mjamzito mmoja  kilichosababishwa  na upungufu  mkubwa  wa  damu  uliotokea  baada ya kupasuka  mfuko wa  kizazi 

 Ailsema katika kipindi cha mwezi Novemba hakukuwepo na kifo  chochote cha mama mjamzito alifariki Dunia wakati wa kujifungua na kabla ya kujifungua 

 Alieleza  vifo  ambazo vimekuwa vikitokea kwenye kituo hicho cha Afya cha Inyonga  vimekuwa vikisababishwa  na  sababu mbalimbali 

 Alizitaja sababu zinazosababisha vifo hivyo vinatokana  na maambukizi baada ya  wajawazito kujifungulia nyumbani  na kutopata  matibabu  kwa wakati 

Pia  vinatokana  na  magonjwa  nyemerezi  kwa  kuchelewa  kupata tiba  ya dawa za  kupunguza   makali ya  VVU
 Alisema vifo hivyo vimekuwa  vikitokana na  na  upungufu mkubwa wa damu  unaotokea   nymbani  baada ya kupoteza   damu  nyingi 

 Songoro  alisema vifo  hivyo pia  vimekuwa  vikitokea  vimekuwa  vikisababishwa  na  maambukizi  baada ya   kujifungua  kufutia upasuaji  baada ya  mtoto kuwa  ameozea tumboni

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment