Home » » HALMASHAURI YA WILA YA MPANDA YAFUNGA MTAMBO WA KUZALISHA KIMIMINIKO CHA NITROJENI WA TSH MILIONI 400

HALMASHAURI YA WILA YA MPANDA YAFUNGA MTAMBO WA KUZALISHA KIMIMINIKO CHA NITROJENI WA TSH MILIONI 400


Na Walter  Mguluchuma
Katavi
 Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  Mkoa ni Katavi  kwa kushirikiana  na  Wizara ya  Mifugo  na uvuvi  imeweza kupa ta na kufunga mtambo  wa kuzalisha  kimiminika  cha Naitrojeni itakayo  tumika   katika  kuifadhi mbegu bora  za mifugo  kwa ajiriya  uhamilishaji  mifugo  wenye thamani ya shilingi milioni 400
 Hayo yalielezwa hapo jana na  Afisa Mifugo wa  Idara ya Mifufo na uvuvi   Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Laulenti Elias  mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  Paza Mwamlima wakati alipo  tembelea   kukagua  mtambo huo wa kisasa uliopokwenye jengo la Idara ya Mifugo na uvuvi Mjini hapa
 Alisema  mtambo huo ililetwa Wilayani Mpanda  mwezi june 2014 na  usimikaji wake ulikamilika  mwezi Septemba  gharama yake umegalimu kiasi  cha shilingi milioni 400 na garama ya usimikaji wa mtambo huo umegharimu kiasi cha shilingi  Tsh37,290,950 na kufanya gharamu kuwa ya jumla ya shilingi milioni  437,290,000kwa mradi huo hadi sasa
 Alifafanua  kuwa mtambo huo wa  Cryomech 120 unauwezo  wa kuzalisha  lita tano  za kimiminika  cha  Naitrojeni  kwa saa moja  kiasi hicho huzalishwa  baada ya  muda  wa kuwa tayari   baada ya mtambo kuwashwa
 Alisema Wilaya ya Mpanda  pamoja kuwa  na idadi kubwa ya  mifugo  iliyopo  bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazo ikabiri Idara ya Mifugo na uvuvi  Wilayani hapa   ambazo alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni
Uzalishaji mdogo  wa mazao ya  mifugo  kama vile  nyama na maziwa ,upatikanaji mdogo  wa mbegu  bora  za mifugo hususani  Ng’ombe
 Changamoto nyingine ni  kuwepo kwa eneo dogo  la malisho  ukilinganisha  na idadi  ya mifugo iliyopo Wilayani hapa   pamoja na  kuwepo  kwa magojwa  mengi ya mifugo  mfano  ndorobo,ndigana  kali na homa ya  mapafu
Nae  Mkurugenzi  mtendaji     wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’ah alisema  mtamba huo ni wanne  kufungwa hapa nchini mitambo mingine kama hiyo ipo katika mikoa ya Mbeya .Arusha na Iringa
Alisema Halmashauri yake imeandaa utaratibu  utakao wawezesha  wafugaji  kupatiwa mafunzo  yatakayo wasaidia  kujifunza nanma ya  kuzalisha  Kimiminika  cha Niaitrojeni
 Alieleza  pia watautumia mtambo huo kwa ajiri  kama mradi kwa ajiri ya wafugaji wa kutoka katika Mikoa ya jirani watakao kuwa wanakwenda kujifunza hapo
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya  ya Mpanda Paza  Mwamlima  aliwataka viongozi wa Halmashauri  kuufanya mradi huu kuwa ni  mradi endelevu
Alisema mradi huo umegharimu fedha nyingi hivyo atashangaa kusikia baada ya muda fulani  mradi huo  kuwa umesimama  sitaki itokea kama ilivyotokea kwa mradi wa mashine  ya  kukoboa mpunga wa Mwamapuli  Tarafa ya Mpimbwe ulivyoshindwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka sita sasa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa