Home » » MARUFUKU LUMBESA KWA WAKULIMA MAANA MNAWAIBIA-MKUU WA MKOA KATAVI

MARUFUKU LUMBESA KWA WAKULIMA MAANA MNAWAIBIA-MKUU WA MKOA KATAVI



Na  Walter Mguluchuma,  Katavi

MKUU wa Mkoa wa Katavi , Dk Ibrahim Msengi amepiga marufu vipimo visivyostahili  vya lumbesa kwa kuwa   wakulima anaibiwa na wafanyabishara wasio waaminifu wenye uchu wa utajiri wa haraka ..

Dk Msengo alitoa marufuku  hiyo wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa  huo  kwamba  kuanzia sasa  vipimo  visivyo sahihi maarufu kama lumbesa marufuku  mkoani humo  kwamba si batili tu lakini pia  vinamwibia mkulima .

Dk Msengi ambaye pia  ni Mwenyekiti wa kikao hicho cha RCC alilazimika kutangaza marufuku hiyo kufuatia taarifa  ya Wakala wa Vipimo  mkoani humo  uliyotolewa mbele ya wajumbe wa kikao hicho .

Ofisa Malalamiko wa Wakala wa Vipimo kutoka makao Makuu , Zainabu Kafunngo  aliwaleleza wajumbe wa kikao hicho  kuwa upimaji  wa vipimo  sahahi  kwa  mazao ya nafaka yakiwemo mahindi katika  soko la  mjini Mpanda  ni changamoto kubwa

Pia wakala hao wamestushwa na uelewa mdogo waliyonayo wakulima  juu ya vipimo  stahiki  ya vifungashio  vya bidhaa zao .

“ Ufungashaji batili  wa bidhaa ni i kinyume cha sheria  lakini hali ilivyo  ni tofauti  kwa mujibu   mapitio ya mwaka 2002 fungu cha 26 ya sherai zetu   ni kwamba tumetoa  utaratibu mzim kwa kila  bidhaa  kufungashwa kwa uzito maalumu  kwa uzito

Isitoshe ikumbukwe kuwa   na maendeleo  tutayapataje  bila kuwa na vipimo  sahihi ….Ufungashaji a mbao  tumeuzoea  kama Lumbesa …. Lumbesa ni nini  ni ufungashaji wa bidhaa ndani ya vifungashio kwa uzito zaidi ya ule  unaokubalika kisheria……

Mbali na uzito huo wa kilo 90 uwe katika  kifungashio  kimoja  sio tena  katika kifungashio  hicho kuwe na kitu kingine  kwa juu  kilichofungwa na kamba  hususani katika magunia  yanayohifadhi  mazao ya nafaka yakiwemo  mahindi

.”  alisisitiza

Aliongeza kwa kutoa mfano kuwa  uzito halali  wa gunia  iliokubalika  kishieria  ndani ya kifungashio ni kilo 90  lakini  hali si  hivyo mkoani humo  ambapo  gunia  moja  la mahindi  linakuwa na uzito wa  kilo 120 .

“Huu ni wizi …mkulima hapa  anaibiwa  kilo  30 kwa kilo gunia  ambao  katika magunia manne  kuna kuwa na zaida ya gunia moja  ambalo lingeweza  kumsaidia mkulima  katika kuboresha  maisha  yake  

ndani ya  vifungashio  kilo 90 linakuwa na kilo 120  wizi mkulima anaibiwa kilo tatu  mane anakuwa na mgunia la ziada  ingemsaidia katika kuboresha maisha yake huu ni wizi mkulima anaibiwa  kilo 30 kwa kila  gunia” anatahadhalisha .

Baadhi ya wakazi wa Mji wa Mji wa Mpanda  waliohojiwa na  mwandishi wa habari  hizi  wamelalamikia  kuwepo kwa udanganyifu  wa vipimo  kwa bidhaa  zinazouzwa madukani  pia  buchani   kutokana  na  kuwepo kwa vipimo  visivyo sahahi  mlaji  anaibiwa kwa kupimiwa  robo tatu ya kilo ya nyma badala  ya kilo moja .
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa