Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mwendesha
pikipiki(BODABODA) aliyejulikana kwa
jina la Zakaria Lungwa(24) mkazi
wa Mtaa wa Kawajense Madukani Wilayani
Mpanda Mkoani hapa ameuwawa kikatili kwa kuchomwa na vifu tumboni na watu wawili
ambao alikuwaakiwafafamu kwa sura na kupolwa pikipiki yake
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari alisema mauwaji ya kikatili
ya Bodaboda huyo yalitokea hapo jana
majira ya saa saba na robo usiku
katika mtaa wa Nselwa Kichangani mjini Mpanda
Alisema
siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa na pikipiki yake ina ya Sanya
yenye rangi nyekundu yenye namba
za usajiri T.752 CQS akiwa huko kwenye maeneo ya
Night Club ilyoko mtaa wa Madini
akiwa kwenye shughuli zake za kila siku
Akiwa kwenye eneo
hilo la Night Club marehemu alipata mteja mmoja wa kiume
ambae alimbeba kwenye pikipiki
yake na kuelekea Mtaa wa Nsemlwa Kichangani
Kamanda Kidavashari alieleza walipofika
katika eneo la Mtaa wa Nsemlwa Kichangani mteja yule
aliyempakia alimuamuru marehemu asimame
katika eneo ambalo hata alikuwa na nyumba yoyote hapo
Ghafla katika eneo hilo alitokea mtu
mwingine mwanaume na
alianza kumwambia marehemu ashuke kwenye pikipiki yake na kisha alimvuta chini pembeni ya barabara
Alisema baada ya kuona hari hiyo marehemu alipiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani
wa eneo hilo hata hivyo hakuweza kupata
msaada wowote kutoka kwa majirani wanaoishi kwenye eneo hilo
Mmoja wa kati ya
watu watu wale wawili alitoa kisu
na kisha alimchoma marehemu tumboni na kisha marehemu alianguka chini na watu hao walichukua pikipiki na kisha walitokomea kusiko julikana huku
wakiwa wamemuacha marehemu akiwa anagalagala chini akiwa anatokwa na damu
Kamanda
Kidavashari alisema marehemu alipata
msaada wa kupelekwa hospitali ya Wilaya ya Mpandabaada ya mtu mmoja aliyekuwa
akpita kwenye eneo hilo akiwa na gari lale alipomwona marehemu akiwa
anagalagala pembeni ya barabara
Alisema marehemu baada ya kufikishwa katika
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda alianza
kupatiwa matibabu na wakati akiwa anaendelea kupatiwa matibabu ambapo
ilipofikia majira ya saa kumi na
mbili jioni alifariki Dunia
Kidavashari
alieleza Jeshi la Polisi linamshikilia mtu mmoja
anaejulikana kwa jina la K
halid Seif (24) Mkazi wa Mtaa wa
Nselwa kuhusiana na tukio hilo
ambae anadaiwa kuwa alionekana katika eneo hilo la Night C lub
akiwa na mteja aliyeondoka na marehemu
Alisema hata
hivyo jeshi la polisi linaendelea na upelelezi
ilikubaini watuhumiwa wa
walihusika na mauwaji hayo ya kikatili
Kamanda
Kidavashari ametowa wito kwa madreva
wote wa Bodaboda wa wa Mkoa wa Katavi wanapoona
kumekuwa usiku kama wamepata
mteja basi wawe
wanakuwa madreva wawili wanaongozana
ili kuweza kusaidiana
kama kutatokea tatizo lolote
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment