Na Walter
Mguluchuma
Katavi
jumla ya watoto
52 wenye umri wa chini ya miaka mitano wameferiki Dunia Wilayani Mpanda Mkoani
Katavi katika kipindi cha miezi sita cha kuanzia Januari
2014 hadi juni mwaka huu kutokana
na sababu mbalimbali ikiwepo upungufu wa
damu
Haya yalielezwa hapo jana na Muuguzi mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Pius Buzumalle wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake
Alisema
jumla ya watoto 52 wenye umri wa chini ya miaka mitano wamefariki
Wilayani Mpanda kutokana na maradhi
mbalimbali yalisababisha vifo vya watoto
hao
Alifafanua katika
mwezi Januari watoto 19 walifariki Dunia kutokana na ugonjwa wa malaria kupanda kichwani
kuishiwa maji mwilini baada ya
kuharisha na kuishiwa damu
Alisema mwezi Februari walifariki Dunia watoto 15
kutokana na ugonjwa wa malaria
kuishiwa damu na kutokana maambukizi
kwenye damu
Mwezi machi walifariki watoto
wanne vifo ambavyo vilisababishwa na kuishiwa maji
baada ya kuharisha mfululizo kwa muda mrefu
na kuishiwa damu mwilini
Muuguzi Mkuu Pius Bumamalle alieleza kuwa mwezi Aprili walifariki watoto nane vifo ambavyo sababu
za vifo hivyo vilitokana na
malaria kupanda kichwani , upungufu wa damu na
kuishiwa maji mwilini
Alisema
mwezi mei na mwezi june
walifariki watoto sita vifo ambavyo
vilisababishwa na upungufu wa
damu na maji mwilini ,kuharisha na malaria kupanda kichwani
Alieleza
kuwa Idara ya Afya katika Wilaya ya Mpanda inaendelea na mikakati
mbalimbali ya kuokowa vifo vya watoto na
mama zao
Aliitaja baadhi ya mikakati hiyo ni wanaendelea kuwaelimisha wazazi kwa kuwahamasisha kuwapeleka watoto wao Hospitalini pindi tuu wanapo kuwa wamegua na pia
kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye kiliniki
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment