Home »
» MAMA MJAZMZITO AFARIKI DUNIA AKIFANYIWA UPASUAJI WA UVIMBE TUMBONI
MAMA MJAZMZITO AFARIKI DUNIA AKIFANYIWA UPASUAJI WA UVIMBE TUMBONI
MJAMZITO AFARIKI DUNIA
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mwanamke mmoja mjamzito aliyejulukana kwa jina la Sesilia John(39) Mkazi wa Kijiji cha Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amefariki Dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa uzazi kufutia chelewa kupatiwa huduma ya tatizo lililokuwa likimsumbua
Mjamzito huyo ambae alikuwa ni mkazi wa Kijiji cha Usevya alifariki hapo Desemba 2 katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambako alikuwa amepelekwa kwa ajiri ya kupatiwa matibabu zaidi
Kaka wa marehemu huyo Matheo John mkazi wa mtaa wa Kotazi mjini Mpanda alisema marehemu dada yake alifariki Dunia katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda baada ya kufanyiwa opasuaji ulitokana na uzazi
Alisema Dada yake alikuwa anasubmbuliwa na ugonjwa wa kuumwa na tumbo na alipokwenda kwenye kituo cha afya cha Usevya ambapo alipimwa na kuambiwa kuwa anatatizo la uvimbe tumboni
Matheo alieleza baada ya kuambiwa kuwa anatatizo la uvimbe aliandikiwa vidoge vya dawa kwa ajiri ya matibabu hayo ambapo marehemu alianza kutumia dawa hizo alizokuwa ameandikiwa na mganga wa kituo cha afya hicho
Alisema marehemu aliendelea kutumia dawa hizo lakini hakupata nafuu yoyote hari ambayo ilimfanya arudi mara kwa mara kwenye kituo hicho cha afya ambapo waliendelea kumpatia dawa za kuondoa uvimbe tumboni
Marehemu baada ya kuona hari inazidi kuwa mbaya siku hadi siku licha ya kuwa anatumia dawa alizoandikiwa ndugu zake waliamua kumsafirisha na kumpeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya matibabu zaidi
Baada ya kufikishwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda alifanyiwa vipimo na kugundulika kuwa ana ujauzito wa miezi mitano na mimba hiyo imekaa nje ya mfuko wa uzazi
Alisema baada ya vipimo hivyo marehemu alidai kuwa anashangaa kuambiwa kuwa ni mjamzito wakati yeye kwa kipindi hicho chote amekuwa akipata siku zake kama kawaida
Alieleza marehemu na ndugu zake walikubaliana na ushauri wa madaktari wa kumfanyia upasuaji marehemu na ndipo walipomfanyia upasuaji na kukuta mimba hiyo imeisha oza kutokana na kutogunduliwa mapema kwa tatizo hili na kupelekea kiumbe hicho kuharibika na kuoza
Matheo alisema siku hiyo baada ya kufanyiwa upasuaji huo Marehemu Sesilia John alifariki Dunia na mazishi yake yalifanyika katika makaburi ya Nsemlwa mjini Mpanda Mkoani hapa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment