Tuesday, December 16, 2014

WATOTO 52 WENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA MITANO WAMEFARIKI DUNIA KATIKA KIPINDI CHA MIEZI SITA MPANDA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
jumla ya watoto 52 wenye umri wa chini ya miaka mitano wameferiki Dunia Wilayani Mpanda Mkoani Katavi  katika  kipindi cha miezi sita cha kuanzia  Januari  2014 hadi juni  mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali  ikiwepo upungufu wa damu
 Haya yalielezwa hapo jana na Muuguzi mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pius Buzumalle wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
 Alisema  jumla ya watoto 52 wenye umri wa chini ya miaka mitano wamefariki Wilayani Mpanda kutokana na  maradhi mbalimbali  yalisababisha vifo vya watoto hao
Alifafanua katika mwezi  Januari  watoto 19 walifariki Dunia  kutokana na ugonjwa wa  malaria kupanda  kichwani  kuishiwa maji mwilini  baada ya kuharisha  na kuishiwa damu
Alisema  mwezi Februari  walifariki Dunia  watoto 15  kutokana na ugonjwa wa malaria   kuishiwa damu  na kutokana  maambukizi  kwenye damu
Mwezi   machi walifariki  watoto  wanne vifo  ambavyo   vilisababishwa na  kuishiwa maji  baada ya kuharisha  mfululizo  kwa muda mrefu  na kuishiwa  damu mwilini
 Muuguzi Mkuu Pius  Bumamalle alieleza  kuwa mwezi Aprili  walifariki watoto  nane vifo ambavyo   sababu  za vifo hivyo vilitokana na  malaria kupanda kichwani , upungufu wa damu  na  kuishiwa maji mwilini
 Alisema  mwezi mei na  mwezi june walifariki watoto sita vifo ambavyo  vilisababishwa  na upungufu wa damu na maji mwilini  ,kuharisha  na malaria kupanda kichwani
 Alieleza   kuwa Idara ya Afya katika Wilaya ya Mpanda inaendelea na mikakati mbalimbali ya  kuokowa vifo vya watoto na mama zao
 Aliitaja baadhi ya mikakati hiyo ni   wanaendelea kuwaelimisha wazazi kwa kuwahamasisha  kuwapeleka watoto wao Hospitalini pindi tuu wanapo kuwa wamegua  na pia  kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye  kiliniki
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment