Home » » HOT NUUUUZ: MTOTO WA MIAKA 14 ABAKA MTOTO WA MIAKA MTATU‏

HOT NUUUUZ: MTOTO WA MIAKA 14 ABAKA MTOTO WA MIAKA MTATU‏

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi  la Polisi Mkoani Katavi  linamshikilia mtoto   Frenk    Stephano (14) Mkazi wa Kijiji  cha Itenka  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenzake (3) mkazi wa Kijiji  hicho  cha Itenka
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa  Katavi Dhahiri Kidavashari  tukio hilo lilitokea  hapo Novemba 18  majira ya saa mbili usiku nyumbani kwa  wazazi wa mtoto huyo  Kijijini  hapo
Alisema  siku  hiyo ya tukio  wazazi wa mtoto huyo aliyebakwa  walikuwa  nyumbani kwao  wakisubilia kula mlo wa usiku  ndipo walipo mlio  mkali   wa  risasi za bunduki jirani  na nyumba yao
Kidavashari  alieleza  baada ya kusikia mlio huo wa  risasi za bunduki  wazazi wa mtoto huyo  waliamua kukimbia  mbio  na kwenda kujifisha kichana  huku wakiwa wamemuacha mtoto wao  ndani ya nyumba  yao
 Alifafanua wazazi hao baada ya kukaa muda mrefu huko walikokuwa  wamekimbilia kujifisha    na kuona hari imekuwa shwari  waliamua  kurudi nyumbani kwao  ilikwenda  kujua mtoto wao waliomuacha atakuwa kwenye hari gani
 Kidavashari alisema  walipofika nyumbani  kwao waliingia ndani ya nyumba  na kumkuta  mtuhumiwa  Frenk  Stephano  ambae ni  jirani yao  akiwa chumbani   huku   akiwa amelala   kitandani na mtoto huyo
 Alisema hari hiyo iliwashitua sana wazazi wa mtoto huyo  na  walianza kupiga mayowe  ya kuomba msaada  kwa majirani hata hivyo mtuhumiwa huyo aliweza kutoka nje na kukimbia kabla ya majirani kufika kwenye eneo hilo
 Alifafanua   wazazi wa mtoto huyo  walikuta  mahari alipokuwa  amelala mtoto wao  kitandani  huku  akiwa  ametapakaa mbegu za kiume  kwenye sehemu zake za siri  huku akiwa akilia  kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayasikia

Kidavashari alisema  jeshi la polisi  limefanikiwa  kumkamata  mtuhumiwa  na anatarajiwa  kufikishwa  mahakamani  wakati wowote  mara baada ya  upelelezi  kukamilika  ili mtuhumiwa  Frenk  Stephano aweze  kujibu  tuhuma ya ubakaji inayomkabili
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa