Home » » MWANAFUNZI AMEZWA NA MAMBA WAKATI AKIOGA MTONI

MWANAFUNZI AMEZWA NA MAMBA WAKATI AKIOGA MTONI


Na Walter  Mguluchuma
Katavi
Mwanafunzi mmoja  wa darasa la sita shule ya msingi Ugalla  Wilaya  ya Mlele Mkoa wa Katavi  Yohana Ramadhani(14) anasadikiwa  kuwa  ameliwa  na   Mamba wakati akiwa akioga na wenzake  katika  mto Ugalla
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata hiyo ya Ugalla Mohamed Asenga  tukio hilo  la kusikitisha lilitokea hapo  Oktoba  17 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni katika mto huu wa Ugalla
Alisema siku  hiyo marehemu akiwa na  watoto wenzake  kamailivyo kuwa kawaida yake  alikwenda kwenye mto huu kwa lengo la kuoga  huku akiwa na  rafiki zake hao ambao walikuwa wakiishi nae Kijijini hapo
 Alieleza  baada ya kuwa wamefika kwenye mto huo walivua nguo zao na kuziweka kando ya mto  na kisha waliingia  ndani ya mto na kuanza kuoga kwa kuogelea ndani ya maji
  Asenga alisema wakati watoto hao wakiwa wanaendelea  kuogelea alitokea mama mmoja alifika kwenye mto huo kwa lengo la kuteka maji kwa ajiri ya matumizi  ya nyumbani kwake
 Alifafanua wakati akiwa anachota maji mama huyo alimwona  Mamba akiwa   kando ya mto huku akiwa anawavizia  watoto hao waliokuwa wakiogelea pasipo wao kujua kama kuna mamba aliye karibu na wao
Alisema mama huyo  alimlazimu kuwaambia watoto hao waache kuoga  na watoke haraka ndani ya mto huu kwani  amemwona mamba akiwa  pembeni ya mtoto akiwavizia  kuwakamata
 Diwani  Asenga  alieleza  ndipo watoto hao walipoamua kutoka ndani ya mto huo kwa kuhofia  kulimwa na mamba  wakati wakiwa wanatoka  ndipo mamba huyo aliyekuwa  pembezoni mwa mto  alipomkamata Yohane Ramadhan na kuingia nae  ndani ya mto
 Alisema wenzake walipomwona amekamatwa na mamba  walianza kupiga mayowe ya kuomba msaada  huku wakiwa wanashirikiana  na mama  amekenda  kuteka maji  hariambayo  iliwafanya  watu ambao walikuwa karibu na eneo hilo  walifika  na kuanza jihihada za  kutaka kumuokoa mtoto huyo  lakini hawakufanikiwa kwani haweza kumwona wala mamba mwenyewe
Diwani Asenga  alieleza  kuwa mpaka sasa mtoto huyo  haja patikana na uongozi wa Kijiji hicho umeisha towa taarifa kwa Idara ya maliasiri na mazingira  iliwaweze kumsaka mamba huyo  na kumuuwa  ili kuepusha vifo vya wananchi wengine  wa Kijiji  hicho
Mwisho
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa